Nimesikiliza kipindi hicho cha njia panda ambapo wanandoa Toby na Tausi wana mgogoro au ugomvi, wameshirikisha wazazi imeshindikana ndio Tausi kaja redioni anasimulia hadi mambo ya ndani kabisa loh! Binafsi nimeona si sahihi kuelezea mambo hayo redioni, ni kujidhalilisha tu! Lakini sijajua wanatakiwa wayajadili wapi kama wazazi wameshindwa!
Sio sahihi hata kidogo. Kutangaza kupitia redio mambo ya ndoa sio sahihi na hayo siyo matanngazo ya mpira.
Upatanishi wa mambo ya ndoa unahitaji hekima na utulivu kwa wachache wenye sifa hizo, kuanika udhaifu wenu kwa kila mtu ni kujichimbia handani litakalo ifukia na kuizika ndoa kabisa.