CLOUDS FM MJIBUNI MSAFIRI DIOUF BHANA!

Tarishi

Senior Member
May 9, 2008
103
133
Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha 360 cha Clouds FM ambacho kwa kuwa ni Ijumaa leo hujikita katika michezo na burudani, na wageni walikuwa bintiye mtangazaji Gadna G. Habash, Karen, na rapa wa Twanga Pepeta, Msafiri Diouf.
Huyu Diouf ndiye aliyenifanya niangalia kipindi kizima maana alikuwa ameshanichefua kwa kuvaa pama na miwani ya jua na headphones (!) akiwa studio (sijui ushamba wa kujifanya wa-Congo wanamuziki wetu wataacha lini). Nikataka nimsikilize kila neno atalosema ili nimpime kama anazo za kumtosha kichwani au dishi limekaa vibaya.
Uongo mbaya, ukiondoa mavazi aliyovaa na vikorokoro vingine kiasi cha kuonekana hamnazo, Msafiri Dious alini-impress vibaya sana kwa kuweza kuongea kwa namna ambayo ni watu 'vichwa' tu huongea na kujibi maswali. Nilighadhabika kwa nini wamchanganye Diouf na kinda kama Karen ambaye naona Clouds na baba yake wanafanya juu chini apande chati. sina uhakika kama watafanikiwa maana kama ni yes ni yes tu, na kama ni no ndio hivyo tena..
Ah, tuyaache hayo. Turudi kwenye mada yangu ambayo ni kuiomba Clouds FM imjibu Msafiri Diof kwa swali alilomuuliza mtangazaji Hassan 'Tanzanite" Ngoma kuhusiana na uteuzi wa vikundi vinavyofanya maonesho wakati wa tamasha la Kila mwaka la Fiesta.
Badala ya Msfairi Diouf kujibiwa, na Hassan akionekana kabisa kufedheheka na kukosa la kujibu, ghafla likaibuka tangazo na kufuatiwa na lingine na lingine tena na hata Hassan Ngoma aliporudi hewani, tukawa tunamuona Q Chilla na jamaa mmoja hivi. Msafiri Diouf na Karen Habash hawakuwepo.

Msafiri Diouf aliuliza: Hivi wasanii wanaoteuliwa kufanya maonesho ya tamasha la Fiesta ni wa Bongo Fleva peke yake ama hata wale wa muziki wa dansi wanaofanya vizuri pia wanaalikwa?

Kwa nini Diouf hakujibiwa?

CLOUDS TUPENI JIBU TAFADHALI
diouf saluti5.jpg
 
Ngoja aka google (kidding :D). Nadhani lilikuwa swali ambalo hakulitegemea, awe anajipanga anapoalika watu kwenye interview.
 
nafatilia sana clouds mara nyingi hua ni wazito kujibu maswali yanayowahusu
nakumbuka waziri wa mazingi january makamba aliwahi kuwauliza watangazi wa kipindi cha brakfast
kwanin nyie clouds radio yenu inamatangazo mengi sana
majibu yao sidhani kama yalijitoshereza.
asante mkuu hao ndivyo walivyo
 
Pia aliuliza ni kwanini clouds hamchezi nyimbo za wasanii waliopo chini ya Wasafi? Wakati hasani ngoma anajibu umeme ukakatika dah.kidng
 
Baada ya mwana masanja banza stone. Msafiri diof ndio rapa Namba mbili kwa mtizamo wangu. Ila unga tuu una tuhalibia vijana. Niliwahi msikia asha baraka akisema pia moja wa rapa mwenyekipaji diof
 
Msafiri pia alipoulizwa kuhusu kutumbukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na nini ushauri wake ,alijibu kuwa hana comments.

Anaonekana bado stimu ziko kwenye damu.

Makorokoro kibao studio naona bado dishi alijakaa sawa.
 
Msafiri pia alipoulizwa kuhusu kutumbukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na nini ushauri wake ,alijibu kuwa hana comments.

Anaonekana bado stimu ziko kwenye damu.

Makorokoro kibao studio naona bado dishi alijakaa sawa.
Msafiri pia alipoulizwa kuhusu kutumbukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na nini ushauri wake ,alijibu kuwa hana comments.

Anaonekana bado stimu ziko kwenye damu.

Makorokoro kibao studio naona bado dishi alijakaa sawa.
Ngada iliathiri sauti na ubongo
 
Back
Top Bottom