Jamani natambua umuhimu na jukumu la kutoa habari na burudani hasa kituo bora kabisa cha Clouds, ila tu nadhani jamaa wana matangazo mengi sana yani yakianza ni dk 10 bampa to bampa matangazo. Sijakataa uwepo ma matangazo maana ndo yanayowalipa ila tu nadhani yanapozidi namna hii inaboa.
Redio saivi haisikiliziki, yani asilimia karibu 90% ya content ni matangazo tena yanajirudia hadi kinyaa, watangazaji wakiwasha mic kila mmoja anasoma tena tangazo lake wakimaliza wanaongea mazungumzo nonsense tupu afu wanarudia kupiga matangazo na mapambio. Yani hata hao watangazaji nadhani hawajitambui udhalilishaji wanaofanyiwa na mabosi wao wanasema wingi wa matangazo ndo kipimo cha success kumbe wasikilizaji wanapukutika kila uchao.