Hili ni halina ubishi, clouds wana fanya hivyo sababu ya kubania wasanii walio kua wanaonekana kufunuka kimikataba, hawa jamaa huwa wakisha kuona una ufahamu fulani au hata umepeleka cd yako kwenye kituo kingine kabla ya wao basi hawata piga nyimbo zako na ndio maana nyimbo ni zile zile tuu.
Ruge ana influence kubwa sana katika hii biashara ya musiki na anapo taka kuku bania ana weza kukufunggia popote , kuanzia kwa muhindi mbaka kwnye radio na TV , huyu jama ni kikwazo kikubwa kwa ajira za vijana, kiasi cha kuwafanya hata wafanyakazi wake wawe kama yeye katika masuala ya ku cheza nyimbo zao Redioni.
Jk alisikiliza ile risala ya RUge ikisomwa na Lady JD kuhusu kufungua proffesional mastering studio na baada ya muda mfupi wakakaa kikao na kuchaguana wao wenywe bila kushirikiana na wengine ,ambapo lady JD ndio mwenyekiti .
Na habari mitambo imefika teari na hiyo studio ni itakua chini ya usimamizi wa RUge , je hapo kuna usalama kwa wasanii wengine wasio chini ya Ruge?JK alifikilia nini bila kushirikisha wadau kujua , huu mchango anao toa uta simamiwaje?
Kazi kubwa na safari ndefu kwa wasanii na ukizingatia clouds wamesha wakamata hawa marketing maneger wote kuanzia kina Kevin Twissa na wengine wote .Labda mbaka kuwe na sys ya kucheki ratings za vipindi kuona kipi kina wasikilizaji wengi labd ahapo itasaida ila bado l suala la kua indpendent , kuto ingiliwa na pia hawa watu wa market watatoa report gani kwa ma bosi wao ili waweze toa pesa kwa walengwa .Bila hivyo Ruge ataendelea kua kiboko yao!