Clouds 360 wamepotosha kauli ya Kamanda Mpinga

Clouds 360 wamepotosha kauli ya Kamanda Mpinga

TumainiEl

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
7,266
Reaction score
14,274
Kwenye kipindi cha 360 kamanda Mpinga alisikika akipiga marufuku chama cha kutetea abiria kufanya shughuli mikoani na badala yake wafanye kazi ya kuwaelimisha raia kwenye stand kuu Dar. Pia akasema chama hicho kazi yake ni kuekumisha na sio kusimamia sheria kwa sababu jukumu lakusimamia sheria ni la jeshi la polisi.

Baada ya kumaliza kusema watangazaji wa clouds wakaanza kuichambuwa hiyo kauli. Cha kushangaza badala ya kusema kauli ya kamanda Mpinga wakaja na uchambuzi tofauti na nitanukuu:
Mtangazaji wa kiume: Kamanda Mpinga amekosea kwa sababu hana mamlaka ya kukifuta chama akaenda mbali zaidi na kumuuliza mwenzake hivi kweli kamanda Mpinga ana haki ya kisheria kukifungia chama?

Kiuhalisia clouds 360 wamepotosha, kamanda Mpinga hajakifungia chama hiki bali amesimamisha shughuli zao mikoani na kuagiza wafanye kazi zao stand kuu. Pia amewaasa kutosimamia sheria ila kutoa elimu kwa wasafiri kama ilivyoainishwa ktk katiba yao.

Kiukweli clouds 360 TCRA fine inawahusu. Reff 360 ya tarehe 23/12/2016 asubuhi.
 
Kamanda mpinga ana mamlaka ya kuwazuia wasifanye shughuli zao mikoani na kuwapangia mahali pa kufanyia kazi zao, tuanze na hili kwanza
 
Clouds wapo kwa ajili ya kumpa sapoti konda, hawa wengine watachafuliwa sana tu.
 
Wewe umezidi kukurupuka sana kama alivyo mkuu ..

Mpinga; "vyama vyote vya mikoa vilivyokuwa vinawatetea abiria vimesitishwa rasmi, na badala yake kile chama cha mkoa wa DSM ndicho kitakachokuwa na uhalali wa kuendelea na majukumu ya kuwaelimisha abiria na si kusimamia sheria.
 
Hakuna wa kuifungia mawingu, mkuluu wetu kawatumia kadi ya X mas
 
Chakua hawatoi elimu wamekuwa wasimamizi wa sheria na tatizo ndo lilipo hapo
 
Kwani hicho chama kimesajiliwa kufanya kazi Tanzania au Ubungo!?
Alafu tatizo lingine ni kuwa hata hawa waliokabidhiwa majukumu ya kitaifa wanaendelee kuamini eti Dar es Salaam ndio Tanzania na matokeo yake nchi haipigi hatua kifikra!
 
Sasa mkuu asubuhi yote hii muda Wa kazi upo kwenye kideo ...
Tatizo watanzania uwa tunafkiri kila mtu anafanya kazi ofsini, au lazima aamke asubuhi aende kazini.
Kumbe wengine walinzi, wanakuwa lindoni usiku na wengine wame invest mashambani wanaenda mara moja kwa week n.k n.k..
 
Back
Top Bottom