Miss Halima
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 302
- 643
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga (21), ameweka rekodi ya dunia ya kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya mpira wa miguu wa wanawake baada ya kusajiliwa na klabu ya Washington Spirit inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Marekani (NWSL), akitokea Al Nassr ya Saudi Arabia.
Luvanga ameweka pia historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kusajiliwa na kucheza katika Ligi Kuu ya Wanawake Marekani (NWSL), baada ya kujiunga na Washington Spirit kwa mkataba wa miaka minne hadi mwaka 2029.
Usajili huo umefanyika kwa ada ya uhamisho ya €1.70M/$2.3M sawa na Tsh. Bilioni 6.081 ambapo msimu wa 2025/26 aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Saudia akifunga magoli 24 kwenye mechi 14 na kutwaa Golden Boot.
Orodha ya wachezaji 10 wa mpira wa miguu wa wanawake waliosajiliwa kwa ada kubwa zaidi duniani (kulingana na picha hizo):
Luvanga anaondoka Al-Nassr baada ya kushinda mataji sita, yakiwemo matatu ya ligi mfululizo, pamoja na Saudi Women's Cup, Super Cup na WAFF Women's Clubs Championship.
Washington Spirit imesema Luvanga ameongezwa kwenye kikosi ili kuongeza chaguc katika safu ya ushambuliaji, huku klabu hiyo ikijiandaa kwa hatua ya playoffs ya NWSL.

| Na. | Mchezaji | Kutoka | Kwenda | Ada ya Uhamisho |
| 1 | Clara Luvanga | Al-Nassr | Washington Spirit | €1.70M |
| 2 | Grace Geyoro | PSG | San Diego Wave | €1.65M |
| 3 | Kerolin | Manchester City 🏴 | Barcelona | €1.50M |
| 4 | Felicia Schröder | BK Häcken | Real Madrid | €1.50M |
| 5 | Lizbeth Ovalle | Tigres UANL | Orlando Pride | €1.30M |
| 6 | Olivia Smith | Liverpool 🏴 | Arsenal 🏴 | €1.27M |
| 7 | Alyssa Thompson | Angel City | Chelsea 🏴 | €1.24M |
| 8 | Jaedyn Shaw | San Diego Wave | NJ/NY Gotham FC 🇺🇸 | €1.07M |
| 9 | Naomi Girma | San Diego Wave | Chelsea 🏴 | €1.07M |
| 10 | Melvine Malard | Manchester United 🏴 | Chelsea 🏴 | €1.00M |