CIF VS FOB

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,283
7,834
Wanauchumi na biashara naombeni tugawane ujuzi. Katika kuhangaikia ununuzi wa mashine kwa njia ya mtandao nimekutana na vitu hivyo.
CIF hii ni cost insurance flight ambayo imeonekana kunifaa kwasababu nachukua mzigo mdogo kwamaana kuwa sio kontena zima. Na kwamujibu wa mkataba huu mnunuzi utapata mzigo wako bandarini. Binafsi natarajia kuagiza powertiller kutoka China aina ya Kubota na nimeanza mazungumzo ya awali.

Ila ambacho sijakielewa ni kuwa mnunuzi nitatakiwa kulipa ghalama zipi tofauti na zile ambazo namlipa muuzaji kwenye mkataba wa CIF?

Kwa mzigo mdogo wa set moja unaweza kutumia FOB contract?

Uzuri ni kwamba katika CIF muuzaji anafanya process mwenyewe na mzigo unakufikia. Hasara ni kuwa kuna baadhi ya vipengere kama kuharibika kwa mzigo uwapo safarini kuwa hasara ya mnunuzi,pia muuzaji anaweza kupanga bei kubwa ya usafirishaji ili apige cha juu.

But under FOB mnunuzi anamtafuta msafirishaji mwenyewe kwa makubaliano maalum.

Mzigo ninaotarajia kuagiza kwa makubaliano ya awali ni US$ 1500 under CIF, je nikilipa hizo natakiwa kuandaa ghalama zipi nyingine?

Natanguliza shukrani
 
Kwema mkuu? Mimi sio mchumi wala mfanyabiashara ila nitajibu kwa kaujuzi kangu kadogo na nitakubali kurekebishwa pale nitapokosea, mkuu ni kwamba FOB huwaga ni actual cost ya bidhaa unayotaka kununua hapo ni mbali na gharama za usafirishaji na bima mfano FOB ingekuwa $1000 basi hiyo ndio ingekuwa gharama halisi ya hiyo powertiller tukija kwenye CIF ndio inakua gharama ya pamoja inayojumlisha gharama halisi za powertiller + usafiri + bima ndio hiyo inaitwa (cost insurance freight) sasa katika manunuzi ukilipia gharama ya CIF maana yake hapo ushamaliza kila kitu ni wao tu wauzaji kusafirisha mzigo wako na ukifika hapa Tanzania itatakiwa utafute agent wa ku clear mzigo wako bandarini ambapo hatua hiyo itaambatana na kumlipa yeye na kulipia kodi ya mzigo wako na kunaweza kuwa na malipo tofauti tofauti kulingana na bidhaa yako mfano kama gari huwa wanalipia port charge sasa sijajua kama na mizigo midogo huwa inalipiwa pia hope, kama utataka kulipia FOB peke yake ili kuokoa hati hati ya kutozwa gharama kubwa kubwa za usafiri kuna uzi humu unajadili kampuni za kitanzania zinazosafirisha bidhaa toka China kuja Tanzania jaribu kucheki nao ili uwaunganishe na muuzaji wa mzigo wako labda inaweza saidia mkuu mbali na hapo sina la nyongeza wenye ujuzi zaidi yangu watakuja nikosoa nilipokosea na kuongezea maelezo zaidi. All the best mkuu.
 
Back
Top Bottom