Ndugu zangu,
Huu sio wakati wa kuwalaumu waislamu au mtu yeyote,(Yesu anasema muwapende adui zenu na muwaombee, Mungu ndie mwenye hukumu ya haki) mwenye macho na atambue ya kuwa, Mwana wa Adamu yu karibu kurudi, huu ni muda wa kutubu, kusali, na kuomba neema kwa Mungu. Na yeyote atakaeliitia jina Bwana(Yesu), ataokolewa. Ushauri, tuombeane sote, kwa wale wanaomuamini Kristo, ili tuweze kuvumilia yale yote ambayo yako mbele yetu, pia tuwaombee wakristo wote walioko duniani. Wapinga kristo ni wengi mno sasa hivi sio tu waislamu, dhambi iko nje nje kila mahali, kwenye internet, redioni, magazetini, mashuleni, vyuoni, through mobile phones, ukatili unaondelea sasa hivi ni wa kutisha, mauaji ya kutisha, njaa,dhuluma, ufisadi, matetemeko ya ardhi, climate change, global warming, extreme weather conditions(snow), flood, vita, na dalili za vita(iran against Israel, USA against North Korea), economic recession, Yesu alisema, mkiyaona hayo, mjue ule mwisho umekaribia, mwenye kujitakasa na azidi kujitakasa. Lakini, neema bado ipo, kila mtu akimuita Yesu, atasemasamehewa dhambi zote.
Tunayoyaona kwa sasa yalikwisha kutabiliwa na manabii, na hayatabadilika ila yatazidi kuwa mabaya mno ili neno lipate kutimia, mambo yote yatapita lakini, neno la Mungu halitapita.
Ukiona kuna negative(-), pia ujue kuna postive(+),ukiona kuna maasi, ujue pia kuna mema, ukiona maasi yamezidi, ujue pia neema ni nyingi mno, ukiona mtu anajitolea kupigania dini, na hata kuua watu, tena kwa kujitoa mhanga, pia tujue hivi yupo mtu mmoja(Yesu), alijitoa mhanga ili watu wauone ufalme wa Mungu, kwa kuwa shetani yupo maana tunaziona kazi zake, pia Mungu yupo hata sasa anazidi kukamilisha idadi ya watu wake. Idadi ikikamilika tu, tutamuona Yesu mawinguni. Pengine ni wewe Yesu alikuwa anakusubiria ili utubu na kumuamini, na atakusamehe.