Chuo kikuu mzumbe Dar campus jalini mda wa wanafunzi

Chuo kikuu mzumbe Dar campus jalini mda wa wanafunzi

french

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2017
Posts
3,648
Reaction score
3,864
Salaam,

Wakuu naenda moja kwa moja kwenye mada. Chuo kikuu mzumbe dar campus kusema kweli huwa hawajali mda wa wanafunzi kwenye utoaji wa matokeo ya research. Mwaka huu mwisho wa kukusanya research reports ilikuwa mwezi wa 8 na matokeo yakatoka around mwezi wa 10. Hapa wanajali mda kwa kujua fika mwezi wa 12 wanafunzi wanahitaji ku graduate. Kuna wanafunzi ambao huwa wanachelewa ku submit na walitakiwa mwisho wa kusubmit mwezi wa 10. Sasa hapa wameongeza tena mda mpaka mwezi wa 12 wakati kuna watu walisubmit mwezi 10. Kwa hiyo hawa wa waliosubmit mwezi wa 10 kazi zao hazisahihishwi wanasubiriwa watu wa mwezi wa 12 nao wakusanye. Na kwa habari nyepesi nyepesi naskia matokeo yatatoka mwezi wa 3. Sasa hii si haki, mtu amepeleka kazi mwezi wa 10 aje apate matokeo mwezi wa 3. Hata kama mtu atagraduate 2019 still transcript mtu anahitaji mapema. Naomba mubadilike mnapoteza sana mda wa watu unnecessary. Mtu hawezi kukaa miezi mitano anasubiri matokeo ya research, au bora tu hizo reserach papers mgeturudishia ili tufanye verification mpaka hiyo 31st december tusubmit wote
 
Back
Top Bottom