Chuo kikuu cha dar es salaam

semausikike

New Member
Apr 10, 2011
4
0
Wadau naomba mnisaidie, nimememaliza chuo kikuu lakini wanakataa kunipa cheti changu kwasababu -nimepoteza vyeti vya kidato cha nne na cha sita.

Je ni tumie njia gani ili Chuo kikuu cha Dar es Salaam kinipe cheti changu? Je kuna njia yoyote ya kisheria ninaweza kuitumia kuwabana ili niweze kupata vyeti vyangu na kuendelea na masomo zaidi sehemu nyingine.

Naomba msaada wenu!
 
Huwezi kupata uthibitisho wa Wizara ya Elimu kwamba umefanya mitihani hiyo na exam number zako?

Na jee transcript yako haitakiwi kuwa na picha yako? Nakumbuka enzi zetu transcripts ziikuwa na picha.

Na ID hukupewa hapo chuoni? Vyote hivyo ni vya kukusaidia kukutambulisha wewe kama ndiyo mmiliki halali wa hivyo vyeti.
 
easy. Wasiliana na shule ulizosomea watoe uthibitisho. Pia waweza tupatia jina kamili hapa hapa ili kucheck online, unless kuna namna 'flani'.
 
Unapopoteza au kuunguliwa na documents kama hizo unaripoti polisi na pia kutangaza kwenye magazeti. Kama ulifanya hivyo peleka vielelezo hivyo chuoni nao watakupa cheti chako.
 
Fuatilia taratibu za kupata vyeti vyako necta kwani ni kweli udsm hawawezi kukupa kwani uchakachuaji ni mwingi mno.......
 
Tafuta results slips/ Hata vyeti vyako visivyokuwa na matokeo za shule zote ulizotoa zikiwemo O'level na A'level huku pia ukiripoti tukio la kupotelewa vyeti vyako polisi na NECTA ili upate uthibitisho kuwa ni wewe kweli.
Pia usisahau kwenda kupata Results slip yako inayoonyesha matokeo mwanzo - mwisho kwenye department hapo UDSM ulikokuwa unasoma.
Jitahidi pia, kutembelea shule ya sheria UDSM onana na wakili yeyote atakusaidia zaidi shida yako.
Pole,

Pasaka njema.
 
Wadau naomba mnisaidie, nimememaliza chuo kikuu lakini wanakataa kunipa cheti changu kwasababu -nimepoteza vyeti vya kidato cha nne na cha sita.

Je ni tumie njia gani ili Chuo kikuu cha Dar es Salaam kinipe cheti changu? Je kuna njia yoyote ya kisheria ninaweza kuitumia kuwabana ili niweze kupata vyeti vyangu na kuendelea na masomo zaidi sehemu nyingine.

Naomba msaada wenu!
Bila shaka ulipopoteza vyeti vyako vya kidato cha nne na cha sita ulitoa taarifa polisi na kutangaza kwenye gazeti la serikali kwa siku 21.
Hapo unatakiwa kupeleka sanduku la barua la Udsm pale NECTA na kuwaambia NECTA watume "Statements of Results" kwenda Udsm.
Kisha ufuatilie Udsm kama watakuwa wamepata hizo statements ..bila shaka watakupa vyeti yako vya chuo.
Sidhani kama unahitaji msaada wa kisheria huu niliotoa hapo ni msaada wa kiutaratibu.
 
Ndugu yangu UDSM wameanza lini kuomba vyeti vya form four na six ukitaka transcript yako na cheti? Sidhani kama wanavihitaji. Ninachojua mimi hivyo hutakiwa pale unapojiunga chuo kikuu baada ya hapo hawavihitaji tena labda kama utaomba kundelea na masomo. Ukimaliza chuo kawaida huwa unafanya clearance ambayo ukiwa unataka cheti chako wanataka upeleke clearance form ikiwa imejazwa na hii haihitaji vyeti vyako vya secondary na kuna form ipo hapo ofisi ya undergraduate unatakiwa uijaze u attach na hiyo clearance form basii unapewa both transcript na cheti,. By the way transcript kawaida ina matokeo yako yoote ya form four na form six. So kama unaomba masters huitaji vyeti hivi. Nina wasiwasi sana otherwise labda wame doubt uhalali wa vyeti vyako wanataka uvipeleke kama ushahidi kama kutakuwa na kesi ya kujibu ndugu. Pole sana!:A S-omg:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom