Yap kipo kinaitwa Lugalo military medical school. kinatoa kozi tatu kuu Clinical Medicine (clinical officer), Nursing (Diploma) na Assistance Medical Officer (AMO). Kozi hizi huchanganya raia na askari kuwa darasa moja na hospital ya mazoezi ni hapo hapo lugalo general military hospital. ni chuo kikongwe sana toka 1980's. kupata form nenda chuoni ofisini kwao. Njia nzuri ya kufika nenda kama waenda lugalo hospital ukifika getini ulizia chuo utaelekezwa usisahau kubeba kitambulisho chako chochote ili utambulike getini. kwa kawaida form hutolewa kuanzia march hadi juni kama sijakosea bei ya kawaida na masomo huanza september kila mwaka. Specifications ni kama za wizara ya afya. kumbuka hiki ni chuo private si cha serikali.