Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 132
Habari nilizopata jana kutoka chuo cha uhasibu Arusha ni kwamba. wanafunzi wa chuo hicho wanampango wa kugoma jumatatu na kuandamana hadi body ya mikopo Dar. Mtoa habari aliniambia kuwa wanafunzi hao wamefikia uamuzi huo baada ya kuishi kwa maisha magumu chuoni hapo bila kupata mkopo kutoka bodi ya mkopo kama walivyokuwa wameahidiwa. Aidha inasemekana kuwa mkopo umetolewa kwa baadhi ya wanafunzi wachache na wengine wengi bado hawajapata bila ya maelezo yeyote kutoka kwa uongozi wa chuo (ambacho kinamilikiwa na Hazina) na pia maelezo kutoka wizara ya elimu ya juu/body ya mikopo. Wanafunzi hao walijaribu kutumia njia nyingi za kiplomasia ikiwa ni pamoja na kuwatuma viongozi wao kwenda Dar kuonana na uongozi wa bodi ya mikopo bila ya mafanikio na ndio maana wameamua kufikia uamuzi wa kugoma.
Kwa wale walioko huko Tz hasa Arusha wanaweza kutupatia habari zaidi.
Mimi huwa naumia sana napoona kuwa serikali yetu haijali elimu. Vipaumbele vyetu vikowapi? vijana wanataka kusoma lakini wanashindwa sasa tusipoelimisha vijana wetu taifa la kesho litaendelea kuwa la wajinga na hatutaweza kuondoa umasikini kamwe.