Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwachafuka, Mkuu wa Mkoa apigwa mawe! Lema asakwa na polisi

mkuu rubi tupo hapa kujenga na watoto wetu wanasoma hizi thread bila kupepesa macho,wala kumung'unya maneno kosa la lema ni nini katika hili sakata?busara ya mulongo iko wapi katika hili tatizo?
Ngoja nikuulize ktu kidogo nilichoona mimi kwenye taarifa ya habari mkuu wa mkoa anafika ile kutaka tu kuongea wanafunzi wanazomea hawataki hata kusikiliza kisa dakika chache zilizopita Lema ametoka kuwaambia wasiwe waoga kwa kuwa ni dhambi mbaya kulikokuua mtu.

Kwa kifupi tu hapo hujaona kosa lililotendeka. wewe kama mzazi mnamfunza nini mtoto wako kuwa kwanza asiheshimu mamlaka. kwa nini huyo Lema kwanza hakutaka kujua kiini cha huyo mwanafunzi kuuwawa na huyo wanayesema mwanakijiji. Hatua zipi alichukua zaidi ya kuhamasisha vurugu. ni mengi ningeongea ngoja nitoke kwanza ila siku zote kwenye fujo waumiao ni hao wahamasishwaji wanaofikiri kwa Masabri. Matokeo yake chuo kimefungwa aliyefaidika ni nani. Ungekuwa wewe ungechukua uamzi gani? kwa yale yaliyotokea jana?

Labda naomba ushauri wako ungekuwa wewe ungefanyaje na hatua zipi zichukuliwe kwa yale yote yaliyotokea Jana itikadi isizingatiwe tafadhali!
 
Back
Top Bottom