Chuo cha IFM na ufisadi kwa vijana wetu

Chuo cha IFM na ufisadi kwa vijana wetu

theHAVARD_product

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
297
Reaction score
211
Wakuu nina mdogo wangu anasoma chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ,mambo aliyonileza kwanza yalinisisimua..SIKUAMINI!

Anasoma Computer Science(BSC) ila kero zilizopo hapo kutokana na ufisadi wa uongozi wa chuo hicho sidhani kama ni nia nzuri kwa maendeleo ya masomo ya vijana wetu hasa katika kipindi hiki cha utandawazi.

Haya ni baadhi tu ya mambo ya ufisadi yanayoendelea chuoni hapo:

1) Hakuna Free Internet services (Wireless) chuoni hapo japokuwa Wanafunzi wa Masomo ya Computer wanalipishwa zaidi ya wengine kwa ajili tu ya huduma hiyo.

Hili linashangaza kwa chuo kutokuwa na Wireless kwa wanafunzi kupata masomo Online.

2) Computer Labs ,computer ni chache na asilima 50% ya computer ni mbovu!!

3)Wanafunzi kulazimishwa kulipia elfu 50 kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima hata kama hawataki.

na Mengineyo....
 
Nakala iende kwa utawala wa chuo.
 
Huyo mdogo wako mwongo,npo ifm mfuko wa afya c lazma na pia internet c kwamba hakuna kabsaa coz maeneo km library na block d watu wanatumia net
 
Haya ni baadhi tu ya mambo ya ufisadi yanayoendelea chuoni hapo:

1) Hakuna Free Internet services (Wireless) chuoni hapo japokuwa Wanafunzi wa Masomo ya Computer wanalipishwa zaidi ya wengine kwa ajili tu ya huduma hiyo.

Hili linashangaza kwa chuo kutokuwa na Wireless kwa wanafunzi kupata masomo Online.

Wanasingizia tu masomo ila ni movie na series.

2) Computer Labs ,computer ni chache na asilima 50% ya computer ni mbovu!!

Hili ni tatizo sugu kwa vyuo vingi TZ. idadi ya miundombinu hailandani na idadi ya wanafunzi.

3)Wanafunzi kulazimishwa kulipia elfu 50 kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima hata kama hawataki.
Kama ana kadi ya bima binafsi anapaswa kuandika barua ya utambulisho wa bima yake na nakala ya kadi yake ya bima, kama hana ni muhimu alipie kwani matibabu kwa dunia ya kileo gharama sana hivyo kwa upande mmoja inasaidia kupunguza gharama anapougua.

Mwisho wa kunukuu hata vyote vingepatikana lalamiko siku zote halikosekani.
 
Huyo mdogo wako mwongo,npo ifm mfuko wa afya c lazma na pia internet c kwamba hakuna kabsaa coz maeneo km library na block d watu wanatumia net

Wewe ni miongoni mwa mafisadi hapo chuoni na wala si mwanafunzi.Unakataa nini wakati mwanangu pia anachukua kozi hiyo hiyo ya computer science and IT kalipishwa 50,000/=?
 
Hata bima unalalamika? Watanzania bhana utafikiri unaliaporo hospital kwako. Hiyo ni kwa faida ya ndg yako.
 
Haya ni baadhi tu ya mambo ya ufisadi yanayoendelea chuoni hapo:

1) Hakuna Free Internet services (Wireless) chuoni hapo japokuwa Wanafunzi wa Masomo ya Computer wanalipishwa zaidi ya wengine kwa ajili tu ya huduma hiyo.

Hili linashangaza kwa chuo kutokuwa na Wireless kwa wanafunzi kupata masomo Online.

Wanasingizia tu masomo ila ni movie na series
Nachelea kuamini kama naww ni fisadi wa hapo IFM kwani mwanafunzi kuangalia series na movie ni mbaya?? ndo anyimwe haki yake ya msingi anayolipia katika Ada???
 
IQ ndogo,IQ ndogo..So waliochangia hapo juu wote ni wanafunzi na wewe pia ni mwanafunzi?? Kwa hiyo unanipangia post ya Kuchangia??

Hapo kwenye Red::A S wink: Dont tell me ,how stupid you are..

Nachukua nafasi hii kukupongeza ndugu yangu una IQ kubwa, ila ukitaka kujibiwa kistaarabu na wewe kuwa mstaarabu, sitaki kuendeleza mabishano na kejeli zisizo na tija, mlalamikaji katoa hoja na nimetumia uhuru wa maoni kuchangia, kwa mtazamo wangu, (sio wako) na pia mimi si fisadi wa hapo IFM.
 
You are....You are Genius,You are Loyal 😛eace:
 
Back
Top Bottom