Chunusi zinanisumbua mwenzenu

Attachments

  • BF6BFF95-5B6D-4FF2-A723-3EAD7B1B0D2D.jpeg
    BF6BFF95-5B6D-4FF2-A723-3EAD7B1B0D2D.jpeg
    460.5 KB · Views: 8
Kwa ufahamu wangu Chunusi husababishwa na mambo makuu mawili...
  • Hormones
  • Changamoto/shida ya ngozi.

1. HORMONES
Mara nyingi sex hormones kama progesterone, testesterone na Oestrogens hupelekea chunusi katika ngozi kwa sababu hormone hizi zinaundwa na kitu kinaitwa Choresterol, hii choresterol ina asili ya mafuta ambayo wakati mwingine hutolewa nje ya ngozi katika mchakato wa utoaji takamwili (excretion) na kupelekea matundu ya jasho kuziba hivyo kutengeneza chunusi..
Process hii ya utokeaji chunusi inafanana na mtu ambae ngozi yake ina mafuta sana.

2.SHIDA YA NGOZI
Wakati mwingine chunusi hutokea kutokana na maambukizi ya vijidudu kama vile bacteria au fangus.

Ni vema ukawaona wataalamu wa ngozi (daktari) kwa ushauri au matibabu kama yatahitajika.
Unaweza kufanya yafuatayo ili kupambana au kuzuia changamoto hio.
  • Oga vizuri kila siku au kila wakati baada ya kufanya kazi inayoshughulisha mwili. Hii itafanya matundu ya jasho kuwa open muda wote.
  • Tumia Maji ya moto (Vuguvugu) kusafisha uso au kuoga.
  • Usipake mafuta mazito usoni
  • Usisugue uso kwa nguvu au kuzitoboa toboa chunusi. Acha zitoke yenyewe.
  • Fanya mazoezi
  • Punguza vyakula vyenye mafuta au vitakavyozalisha mafuta mwilini (punguza vyakula vya wanga)
 
Tafuta hii tube inaitwa Persol 5%gel inapatikana pharmacy upake mara moja kila siku usiku wakati wa kulala…Epuka kupaka mafuta mazito
 
Back
Top Bottom