chungu lakini inamezeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chungu lakini inamezeka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 11, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  sunday kayuni , lakini pia yeye ni kati ya wakufunzi wa TFF na lililo la juu zaidi ya yote kwake ni kwamba ndiye Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho hili la mpira wa Tanzania (TFF).

  Kwa makusudi kabisa nimemkumbuka mwalimu wangu huyu kutokana na hali ya mambo yanavyokwenda katika kandanda ya Bongo. Kayuni amewafundisha wachezaji wengi sana nchini kipindi hicho na wengine sasa ni makocha na bado wengi wao wamepita tena mikononi mwake kama mkufunzi.

  Na wale ambao hawakupata bahati ya kupita mikononi mwake wana taarifa zake zilizo sahihi kabisa kutoka kwa aidha wachezaji au makocha wenzao wa sasa. Kayuni ni mmoja wa walimu
  waliosifika sana kutunza nidhamu ya wachezaji katika timu alizopitia na hata katika timu ya
  taifa wakati alipoteuliwa kuifundisha alikuwa anaisimamia nidhamu kwa hali ya juu sana.

  Wachezaji wote wakijua Stars kapewa Kayuni, basi kulikuwa hakuna wa kuchelewa kupiga
  ripoti kambini, kwani alikuwa haoni hasara kuachana na wewe hata kama ungekuwa fundi kiasi
  gani, lakini hata kama hakuna aliyetokea akachelewa, basi mkiwa kambini kulikuwa na sheria
  zake ambazo hamkuwa na budi kuzifuata, ukienda kinyume nazo unatemwa.

  Hapo ndipo hasa alipoanza kusigana na wachezaji wengi na hatimaye kuanza kumpakazia
  mambo mengi ambayo yamemjengea jina baya sana miongoni mwa wanajamii ya soka, kwani
  wachezaji wengi wa Bongo nidhamu zao sio nzuri.

  Leo anachukuliwa kama mtu mwenye mizengwe na roho mbaya kupita maelezo na mara
  chungu mbovu amehusishwa na tuhuma za kuachwa kwa baadhi ya wachezaji kwenye timu ya
  taifa kwamba ni kwa shinikizo lake ndio maana fulani kaachwa au hakuitwa kwenye timu.

  Mara nyingine misimamo huwa inaleta ‘negative impact’, na hili ndilo linalomkuta Mwalimu
  Sunday leo.

  Lakini nionapo madudu yanayofanywa na wachezaji hawa wa sasa, natamani angepewa timu ya taifa ili atuoneshe nani na nani hawafai kuitwa na wakiitwa iwe ni kwa ‘condition’ zipi, wasipozifuata basi tuachane nao ili kuliepusha taifa na aibu kama za hawa wachezaji walioripotiwa wiki hii kutimuliwa timu ya Taifa.

  Mimi naamini kabisa, Kayuni hahusiki na wala hasimamii uteuzi wa timu ya taifa, na kama
  ingekuwa hivyo mtu mhuni asingepata wapi nafasi ya hata kuitwa kwenye timu pamoja na
  rekodi zake zote za utovu wa nidhamu za siri na dhahiri!

  Inawezekana kutokana na wadhifa wake wa ukurugenzi wa ufundi ana nafasi ya kutoa ushauri baada ya kwisha kuyaona majina ya wachezaji, ushauri si lazima ufuatwe, matokeo yake ‘wahuni’ wanaitwa na wanatuharibia taratibu za mpira.

  Hiki kilichotokea ni zao la kuendekeza ushikaji katika kuteua wachezaji wa timu ya taifa na kuacha taratibu zinazoeleweka. Kama taratibu zingefuatwa, sioni nafasi ya wasio na nidhamu
  katika timu ya taifa kwa sasa iwe ya Bara au ya Muungano, huo ndio ukweli na kama kuna mtu inamuuma na iwe hivyo.

  Timu inateuliwa kwa kufuata rekodi za mchezaji katika klabu yake, kwa maana ya kiwango cha wakati uliopo na rekodi za kinidhamu, wapi ipo nafasi ya wahuni?

  Kiwango cha mchezaji kwenye klabu yake kimepungua sana, imefika hatua kocha wake akawa hamtumii mara kwa mara kama mchezaji wa kuanza, badala yake akawa anaingia akitokea benchi na mara nyingi kama sio zote hakuwa na madhara kwa wapinzani.

  Na suala la nidhamu mtu anafahamika ni ziro kabisa na Tanzania nzima tunalijua hili, ila
  kwakuwa ni mshikaji na timu wamepewa washikaji, basi wacha aitwe ‘awasute’ wasiompenda,
  kilichotokea ni aibu kwake na washikaji zake.

  Huyu mwingine hali kadhalika ni mmoja kati ya wachezaji wanaosemekana kuwa na nidhamu
  mong’onyofu na watumizi wazuri wa ‘majani’, ila kwa kuwa ni mtoto wa maskani nae anaitwa ili ‘wana’ waridhike.

  Haya ni mambo ambayo hayana tija na yamepitwa na wakati, kocha yeyote makini
  asingeweza kuyaruhusu yatokee hata mara moja chini ya utawala wake. Ni kweli Kayuni anaweza kuwa na matatizo yake kama binadamu, lakini kwa hili la kusimamia nidhamu tumpe haki yake, jamaa alikuwa na hadi sasa anaweza ila hatumpendi.

  Tunaowapenda sisi ni hawa wanaoleta ushikaji kwenye timu ya nchi inayogusa watu wote.
  Wachezaji wa Bongo wengi nidhamu zao za kuunga-unga, lakini kwa hili la wiki hii wamevuka
  mipaka, na kama hali ndio hii nadhani wachezaji wetu hawajui thamani ya kuvaa jezi yenye rangi ya Bendera ya Taifa na kuimbiwa wimbo wa Taifa (Mungu ibariki) kabla ya mechi.

  Kama Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde alitoa rai kwa Spika wa Bunge, kuwa wabunge
  wapimwe akili zao kabla ya kuingia bungeni kutokana na tabia zao, basi ni heri pia kama
  tutapima wachezaji wetu kabla ya kuitumikia timu yetu ya Taifa, usikute tunaita ‘wendawazimu’ kwenye timu.

  Ukweli ndio huo, ni Chungu lakini Dawa hakuna budi kuimeza tu!
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  boban/taita?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Teeehteeeehhh sijasema mie
  nurdin abbubakar athman manyupa loh aanajiluza iwapo mchezaji machupa antumia hela kurubuni mke wa mchezaji mwenzie je kurubuniwa na viongozi wa timu za taifa za nje kazi rahisi sana mtu kama huyu
  kale kachezaji cha yanga shamte ali kamelalama sana mkewe bado anatumiwa msg za mapenzi usiku na athuman machupa laana wachezaji hawa wpaimwe akili walaaaaaaiiiii
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwani walifanyaje?
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu ule mtanange wa Rwanda vs Uganda ulivyokuwa mtamu?
   
Loading...