Chumba cha baba kisicho na hadhi yake

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,646
Habari zenu waungwana.

Siku zote huwa tunaamini chumba anacholala baba huwa ni bora kuliko vyote. Lakin kwenye nyumba yetu ni tofauti,maana chumba cha baba kinazidiwa na vyumba vingine.

Chumba cha baba kinazidiwa kwa sababu zifuatazo:
1.Chumba cha baba hakina maji ya kutosha ingawa kuna siku baba alisema maji yapo ya ziada
2.Hakuna mwanga maeneo mengi ya chumba ingawa wasimamizi wa baba wanadai wana mpango wa kuweka hivi karibuni na baba alituambia umeme unatosha na kuna akiba kama 40(nguvu ya kuendeshea umeme.
3.Wasimamizi kwenye sekta ya vitabu hata hawafanyi kazi ipasavyo wamebaki kutishia tu wale wasimamizi wa wasomaji huku wakisema wanahitaji kuona usomaji(ufaulu) unaongezeka
4.Njia nyingi za kuingia chumban kwa baba ni mbovu na hupitika kwa shida
5.Hakuna watumishi wa kutosha wa kufanya kazi chumbani kwa baba
6. Na mengine mengi

Nasikia baba anataka ahamie kwenye nyumba yake hii na atafikia kwenye chumba chake hiki nashauri waboreshe chumba hiki ili kiwe na hadhi ya baba anayostahili
 
Miradi ya maji haikupewa kipaumbele baada ya uchaguzi. Sasa hivi makandarssi wanatemeshwa cheche kisa uchaguzi umekaribia.
Ni sawa na aliyoimba Mpoto "wanatupima viatu mwaka huu,baada ya miaka mitano wanauliza mlisema mnavaa viatu vya aina gani.."
 
Kwahiyo baba amakosa pesa ya kuweka mwanga na mfumo wa maji chumbani au anataka kutuaminisha yeye pia ni mnyonge mwenzetu?
 
Hapa nadhani tatizo si baba ni watu aliowapa wasimamie kwenye asili yake anakotokea baba mambo ni mazuri
 
Mkuu hilo dua laweza kukupa 'presha' tu bure.

Umekwisha kufanya utafiti ktk maeneo mengi nchini na kuona kuwa kawachosha?

Mimi huwa sichangii mada kama hizi kwenye mikusanyiko, mfano kwenye usafiri, magenge ya kahawa nk nk , lakini jumbe ninazozipata, zinafanana sana kimisimamo walionao raia wa kawaida juu ya utawala huu.

Nikisikiliza hoja na michango ya walio wengi, inaonesha dhahiri kuwa jamaa anakubalika kuliko unavyodhania!

Na mwakani atashinda hata bila kampeni kwa % za kufuru.

Ni samaki sangara aliyekwisha jikaanga kwa mafuta yake mwenyewe, hahitaji maneno kusadikisha watu.

Labana akijaalia shahidi kushuhudia niliyoyasema utakuwa ni wewe.
 
Tatizo la hili taifa ardhi yake imebeba mazwazwa wengi sana Ambao uwezo wao wa kufikiri hauwezi kuyaona hayo madhaifu uliyo yaeleza ....na bado Wana muona huyo baba kuwa nimkombozi wao
 
Ni kweli ila ukisoma kwa makini post hii utagundua sijalenga eneo kubwa kuna sehemu naizungumzia,soma paraghaph ya mwisho utaweza kujua wapi nazungumzia
 
Tatizo la hili taifa ardhi yake imebeba mazwazwa wengi sana Ambao uwezo wao wa kufikiri hauwezi kuyaona hayo madhaifu uliyo yaeleza ....na bado Wana muona huyo baba kuwa nimkombozi wao
Na hii ni kwa sababu "binadamu husikia kile anachotaka kusikia tu" ukileta tofauti na anachotaka kusikia hamuelewani
 
Habari zenu waungwana.

Siku zote huwa tunaamini chumba anacholala baba huwa ni bora kuliko vyote. Lakin kwenye nyumba yetu ni tofauti,maana chumba cha baba kinazidiwa na vyumba vingine.

Chumba cha baba kinazidiwa kwa sababu zifuatazo:
1.Chumba cha baba hakina maji ya kutosha ingawa kuna siku baba alisema maji yapo ya ziada
2.Hakuna mwanga maeneo mengi ya chumba ingawa wasimamizi wa baba wanadai wana mpango wa kuweka hivi karibuni na baba alituambia umeme unatosha na kuna akiba kama 40(nguvu ya kuendeshea umeme.
3.Wasimamizi kwenye sekta ya vitabu hata hawafanyi kazi ipasavyo wamebaki kutishia tu wale wasimamizi wa wasomaji huku wakisema wanahitaji kuona usomaji(ufaulu) unaongezeka
4.Njia nyingi za kuingia chumban kwa baba ni mbovu na hupitika kwa shida
5.Hakuna watumishi wa kutosha wa kufanya kazi chumbani kwa baba
6. Na mengine mengi

Nasikia baba anataka ahamie kwenye nyumba yake hii na atafikia kwenye chumba chake hiki nashauri waboreshe chumba hiki ili kiwe na hadhi ya baba anayostahili
Tumechoka na mafumbo yenu....be straight...mnatumia ID fake...bado na mafumbo juu....kama ndio kujificha kiasi hiki...basi ni haki baba yenu kukaa gizani
 
Fumbo huwa kwa kitu ambacho hukijui na hakijakugusa ila kwa waliokutwa na jiwe lilipotupwa gizan wanaelewa.
 
Back
Top Bottom