Tajirimsomi
JF-Expert Member
- Jan 12, 2017
- 4,824
- 5,580
CHUKUA HII
Jamaa wamevamia benki kuiba, mkubwa wao akawaambia wateja wote na wafanyakazi ndani ya benki: Laleni chini na kila mtu atulie jinsi alivyo. Hela ni mali ya serikali, uhai ni mali ya Mungu. Nyie hamna chenu. Kila mtu akasalimu amri akalala chini. Hiyo inaitwa: "Falsafa ya kubadili fikra za watu". Baada ya muda dada wa reception pale benki akajaribu kutaka kuongea kitu kwa sauti. Jambazi likubwa likamwambia: Hebu tulia. Huu ni wizi, hakuna mtu amekuja kubaka hapa. Hiyo inaitwa kuwa "Kuwa profesheno, fuata ulichotumwa tu!". Baada ya kuiba na kuondoka, walipofika nyumbani jambazi mdogo (ambaye alikuwa msomi kidogo) akamwambia yule mkubwa: Tukae tuzihesabu hizi hela. Jambazi mkubwa (ambaye aliishia darasa la nne) akajibu: Ili iweje? Subiri taarifa ya habari jioni watatangaza tumeiba shilingi ngapi. Hiyo inaitwa "Uzoefu". Siku hizi uzoefu ni bora kuliko lundo la vyeti vyako.
Huku benki baada ya wezi kuondoka meneja wa benki akamwambia msimamizi wa tawi: Ita polisi haraka. Meneja wa tawi akamjibu: Subiri kwanza boss, tuchukue milioni kama 100, tuchanganye na zile milioni 300 tulizoiba kiujanja ujanga kwenye mahesabu. Hiyo inaitwa "Changamkia dili kipritenda". Geuza msiba wa wengine kujipatia manufaa binafsi.
Usiku wa siku hiyo kwenye TV ikatangazwa kwamba majambazi wamevamia benki na kuiba Tshs. millioni 500. Yale majambazi yakahesabu na kuhesabu lakini kila yakihesabu yanakuta yana milioni 100 tu! Majambazi yakaanza kulalamika: Yaani kazi yote tuliyofanya, wale wahuni wa benki wao wamechukua hela huku wamekaa tu! Inaonekana ni bora kuwa na elimu kuliko kuwa mwizi! Hiyo inaitwa "Elimu ni bora kuliko mali."
Swali: Nani mwizi hapo?