Chuki Simba na Yanga

Apr 19, 2023
41
89
Yaani hata sijui niielezee vipi mnielewe. Watu wazima kabisa, nchi moja wanakuwa na chuki zisizoelezeka ambazo haijulikani zimeanzia wapi na zitaishia wapi. Yaani wa Yanga wanaichukia Simba, na wa Simba wanaichukia Yanga.

Bado najiuliza je shida ni uwezo wetu sisi ngozi nyeusi au tatizo ni nini?

Najua wewe unayesoma hapa ni mmoja wapo. Hebu jitafakari, chuki hiyo uliyonayo dhidi ya timu pinzani, je umeitoa wapi?

Ilikuwaje ukaichukia timu nyingine huku ukijificha kwenye kichaka cha utani wa jadi?

Nini kifanyike ili michezo katika nchi yetu itujenge tuwe na umoja wa kitaifa na sio uadui kama ilivyo hivi sasa?
 
Ni kwamba haujui mpira au nini?
Barcelona wanawapenda Madrid?
Man u wanawapenda man City?
Arsenal wanawapenda Tottenham?
River plate wanawapenda boca junior?
Inter Milan wanawapenda ac Milan?
Everton wanawapenda Liverpool?
Al ahly wanawapenda zamalek
Wydad wanawapenda raja Casablanca?
USHABIKI NI UCHIZI
 
Kila siku mlikuwa mnaanzisha thread za kuiponda yanga je ulikuja kukemea?
Iweje baada ya kufungwa na wydad unaleta ngonjera zako?
Hapa sipo upande wowote mkuu, nashangaa tu inakuaje hapa bongo unakuta kuna mashabiki wa medeama? Au wa wydad? Ina maana hatupendi nchi yetu iwe na mafanikio kwenye mpira? Watakuja al hilal na tp mazembe watapata mashabiki wa kutosha kwa mkapa ila kwa sisi wabongo dah support kwa timu ikiwa inawakilisha nchi hakuna kabisa
 
Ni kwamba haujui mpira au nini?
Barcelona wanawapenda Madrid?
Man u wanawapenda man City?
Arsenal wanawapenda Tottenham?
River plate wanawapenda boca junior?
Inter Milan wanawapenda ac Milan?
Everton wanawapenda Liverpool?
Al ahly wanawapenda zamalek
Wydad wanawapenda raja Casablanca?
USHABIKI NI UCHIZI
Mkuu hata kama una jirani yako na humkubali kabisa, akipata changamoto huwezi kushangilia hadharani kama inavyotokea hapa Tanzania. Na huu ujinga naamini umekolea zaidi hapa Tanzania na ukichochewa zaidi sana sana na wasemaji.
 
Yaani hata sijui niielezee vipi mnielewe. Watu wazima kabisa, nchi moja wanakuwa na chuki zisizoelezeka ambazo haijulikani zimeanzia wapi na zitaishia wapi. Yaani wa yanga wanaichukia simba, na wa simba wanaichukia yanga.

Bado najiuliza je shida ni uwezo wetu sisi ngozi nyeusi au tatizo ni nini?

Najua wewe unayesoma hapa ni mmoja wapo.
Hebu jitafakari, chuki hiyo uliyonayo dhidi ya timu pinzani, je umeitoa wapi?

Ilikuwaje ukaichukia timu nyingine huku ukijificha kwenye kichaka cha utani wa jadi?

Nini kifanyike ili michezo katika nchi yetu itujenge tuwe na umoja wa kitaifa na sio uadui kama ilivyo hivi sasa?
Mkuu bila upinzani mpira hautakuwa na maana. Ndio maana wanaitwa watani wa jadi.
 
Kumbe unanifahamu mkuu, sema mi mweusi ila upara kama gamondi.


Cha msingi tubadilike, kila timu ipambane na malengo yake. Biashara ya wasemaji wa hizi club kuanzisha vijimaneno vyao hapa vya kutujaza chuki visitufanye tusiwe wazalendo kwa kuipenda nchi yetu.
Mkuu, bila kupeana changamoto hizi timu zingebweteka. Binafsi ninaamini Simba na Yanga zimepandisha viwango vyao kwa sababu ya kuzomeana na kila moja kutaka kuipiku nyingine kimafanikio.

Ukweli ni kwamba hakuna uadui kati ya mashabiki wa Simba na Yanga, ni utani tu na ndio maana hatujawahi kusikia watu wamedhuriana uwanjani au huko mitaani. Mpira ukiisha watu watataniana kisha kila mtu anaenda kwao kulala. Na ndio uzuri wa mpira. Vinginevyo itakuwa kama mko kwenye nyumba ya ibada.
 
.
P-IMG-20231210-WA0070.jpg
 
Back
Top Bottom