Chui aua askari wa wanyamapori Mwanza

Chui aua askari wa wanyamapori Mwanza

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Askari mmoja wa idara ya wanyamapori ( TAWA) anaefahamika kwa jina la Enock Rugaimukamu Gration mkazi wa Pasiansi wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza amefariki dunia mara baada ya kujeruhiwa na chui katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Dcp Wilbroad Mutafungwa amesema askari huyo alijeruhiwa na chui huyo siku ya tarehe 30.08.2025 majira ya saa saba mchana wakati akiwa katika jitihada za kumdhibiti mnyama huyo ambae alikua anavamia makazi ya watu katika kijiji cha Iyago kata ya Mahina wilaya ya Nyamagana ambao baada ya kupata majeraha hayo alikimbizwa Hospitali ya rufaa ya kanda Bugando lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia wakati akiwa njiani kuelekea hospitali.

Screenshot 2025-09-04 002915.png


Katika hatua nyingine Mutafungwa amesema katika tukio hilo askari wengine wawili walijeruhiwa na chui huyo sehemu mbalimbali za miili yao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho cha Iyago wamewapongeza askari wa idara ya wanyamapori (TAWA) kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi kufanikisha kumdhibiti na kumuua chui huyo kwani alikua tayari ameshawajeruhi wananchi wa mtaa huo na alileta taharuki wa wananchi wa mtaa huo.

Kufutia tukio hilo jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari katika maeneo hatarishi na pale wanapoona kuna viashiria vyovyote vya wanyama hatarina watoe taarifa kwa mamlaka husika ili waweze kudhibitiwa.
 
Chui huwa hapendi watu kiherehere kujifanya unamjua sana anakurukia. Chui dawa yake ni kuzuga humuoni na huna time naye
 
Back
Top Bottom