Naam! Umenikumbusha 2000/1 hapo ndani ya Chuchu sound kuna Chuchu Yusuph(rip), Mao Santiago, Hababuu mwana Zanzibar, Omari Mkali, Joniko flower-maua (sasa Machozi band), Gabi Katanga(rip) na wengineo. Walikuwa wapo juu sana miaka hiyo. bendi yao ilivunjika ikiwa bado iko juu-mambo ya mapato. Naamini wanamziki wote waliopitia chuchu bado wanaikumbuka sana bendi yao.
Nikirudi kwenye mada, mi nakushauri ukanunue albamu yao kariakoo au hata pale buguruni unaweza ukaipata. Ndio, kitu kizuri, tuwe tayari kukigharamia, sikushauri uka-burn.