Christian Bella apewa uraia wa Tanzania

Christian Bella apewa uraia wa Tanzania

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,364
Reaction score
18,656
Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva wenye ladha ya R&B na Afro-pop, Christian Bella amepewa uraia wa Tanzania.

1766057086146.png
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene leo Alhamisi, Desemba 18, 2025 ikiwa ni siku ya wahamaji duniani.

Simbachawene amesema Tanzania kuna idadi kubwa ya wahamiaji na baadhi yao wamekuwa wakipewa uraia.

"Sasa anakwenda wapi, amekwisha fika, ameoa hapa, ana watoto hapa na atapata wajukuu hapa. Anafanya kazi vizuri, hana makosa, amefuata utaratibu na muda wote alioishi hapa amelipa malipo stahiki, siyo wengine wanaolanda landa tu,” amesema Simbachawene.

Amesema mtu anaweza kupewa uraia na ukafutwa kama hatafuata utaratibu: “Hatuwezi kumpa uraia mtu ambaye ni hatari ama anayegeuka kuwa hatari, kwa hiyo kuna 'vetting' imefanyika kabla ya mtu kupewa uraia."
 
That's not a big deal at all. Wakongo ni ndugu zetu toka enzi na enzi. Sisi tutaendeleza kupiga spana kwa hao mafala machawa wasanii wa bongo hadi waitukane CCM.
 
Isingekua siyo tabia zake za kitapeli, huyu Bernard Morison nae angeshakua raia
SAVE_20251218_175144.jpg
 
Mwana sana huyu jamaa! Hana adui huyu kwenye maisha yake ya kila siku. Christian Bella, rais ya masauti duniani! You deserve it bro. Umeishi miaka mingi Bongo kwa amani na uzalendo wa hali ya juu. Huna nongwa hata kidogo.
 
Huyu alianzaga kitambo kutafuta uraia mbaka akawa kama analalama hivi kwenye media....kama bado hana mpaka leo hii daaaah
 
Sema haya mambo ni magumu sana kuyaelewa. Kuna wale wachezaji walipewa fasta hadi raia tukashangaa. Na kuna watu inaosemekana wana vitambulisho vya NIDA huku hata kiswahili hawajui.
 
Bado unakaza fuvu tu, fuatilia tulichojadili kuhusu nyoshi sio hivo ulivodhani wewe na uelewa wako wa kukurupuka huo
Ww huna akili, mada inamhusu Bella, comment Yako imekaa kujibu mada inayomhusu Bella mana hujareply Kwenye comment inayomhusu nyoshi.
Ingekuwa umereply comment inayomhusu nyoshi Ndo ungekuwa sahihi
 
Back
Top Bottom