Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,982
- 20,564
Fungua katiba ya CHADEMA sura ya saba 7.2.1, utagundua kuwa hayo yanayofunguliwa nje ya nchi ni magenge ya washabiki siyo matawi ya chama.
Hii inasema hivi:
7.1.2 Ngazi ya Msingi itaundwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika kanuni zilizotungwa
Sasa mkuu unasema kwamba, nakunukuu- "utagundua kuwa hayo yanayofunguliwa nje ya nchi ni magenge ya washabiki siyo matawi ya chama."- mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Lema amekwenda London akiiwakilisha CHADEMA taifa katika hafla ya uzinduzi wa tawi la chama hicho na masharti yoote yamefuatwa.
Hii ndio ngazi ya msingi kabisa kabla ya kwenda hatua ingine ya kuingia pale Tanzania. Na utaratibu alioufanya ndio huouhuo utaratibu ambao CCM imetumia kwenda London na kufungua matawi kadhaa.
Sasa sifahamu umetafsiri vipi kifungu hiki.