Chris Lukosi wa CHADEMA VS Suzan Mzee wa CCM... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chris Lukosi wa CHADEMA VS Suzan Mzee wa CCM...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bull, Aug 8, 2012.

 1. B

  Bull JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema jana wameanza tawi lao la kihistoria hapa Uk kwa kufanya shughuli yao Bar chini ya uratibu wa mwenyekiti wao bwana chris Lukosi wa serengeti Freight. ni jambo la aiabu sana kwa Chama ambacho kinasema kinataka kuchukua madaraka na kwenye mji mkubwa kama London waende kufanya shughuli hiyo Pub.

  Achilia mbali malalamiko ya ndugu zetu waislam waliosema kuwa muda wao wa kufuturu ndio ulikuwa muda wa uzinduzi wa tawi la chadema uingereza.

  pili eneo la bar kwao lilikuwa ni jambo zito.lakini wapo wakristu na hata wasio na dini ambao hawapendi kwenda Bar.kwa akili ya haraka haraka tunapata picha kuwa chadema uingereza ni kundi la walevi ndio maana wakaamua kuwa na shughuli yao Bar tena ya eneo la uswahilini kama ni Tanzania basi kule Tandale kwa mtogole au Mbagala. Wangeweza kwenda hotel katikati ya london ambazo zina kumbi za mikutano na bei yake ni ndogo sana.

  Naomba wana chadema mtuambie kuwa chris ana Elimu gani amesoma chuo kikuu gani hapa UK, tunajua hapa Uk ni kisiwa cha elimu. Ukitizama picha za watendaji wa chadema UK wengi wao wana sura za kilevi na watu waliokata tamaa za maisha hapa UK, wameshindwa kuingia kwenye main stream society ya uk wanaishi maisha ya kighetto.

  Naamini Chadema wameshafeli kwa kumchukua Chris Lukosi ambaye upeo wake ni mdogo na hana tofauti na Susan mzee wa Ccm lakini pamoja na maskendo yake susan mzee bado yuko juuu kidogo ukimfananisha na mwenyekiti wa Chadema Chris lukosi.
  mwenye CV za hawa watu wawili atuletee tuona nani zaidi?
   
 2. B

  Bull JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zetu wa chadema tunaomba Cv za mwenyekiti wenu wa ulaya naona kama mnapata kigugumizi.Mwenyekiti wa chadema Taifa hana elimu nzuri hana hata Diploma na Mwenyekiti wa Ulaya bwana Lokosi ana elimu gani,Mwenyekiti wa Taifa bwana MBOWE tunaweza kusema kuwa hakuishi Ulaya. huyu chris ana elimu ipi? nataka kujiunga chadema kama nitashawishika na uwezo wa chris Lukosi
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Una wivu wa kike..choo cha hapo majuu ni kama ikulu y tzania licha baa.uliwapa dola 5000 kuchukua ukumbi eastern london wakakataa?.YOU ARE LOOSER.wewe ni gamba na nadhani uliitaka iyo nafasi ukawa huna sifa ya ukamanda..pengine ameandaa event,wewe hata mia hujawahi kuwasaidia makamanda..
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba Cv ya mwenyekiti usikimbie swali.
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni loser sio looser nenda shule.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa nchi za wenzetu kufanyia shughuli kama hii ya CHADEMA kwenye pub si kitu kigeni kabisa. Sana sana ninachoona hapa ni ushamba lakini pia kuna tatizo la baadhi ya watanzania wanaokaa nje ya nchi lakini hawajichangi na kujifunza toka kwa jamii zingine. Matokeo yake wanaendeleza majungu yasiyo na tija. Watu wanafanyia tafrija nyingi tu including harusi kwenye pub huko nje, sasa kelele za nini kama sio ushamba? Au mtu akitumia ukumbi wa pub akili zinamruka? Kuna pub ambazo zina kumbi-eneo la kutosha kwa tafrija na shughuli mbalimbali. Kama mtu haujui aulize badala ya kuanika ignorance!
   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wewe ni Gamba gumu ya CDM yanakuhusuje! Wivu wa kigoli.QUOTE=Olympic2012;4395564]ni loser sio looser nenda shule.[/QUOTE]
   
 8. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nadhani Chris kadandia tu train kwa mbele according to siasa za UK opponents walishajua CDM inampango wa mashambulizi lakini hawakutegema dhaifu na iliyokuwa na mikakati ya hovyo namna hile. Wapo wasomi wa kweli na CDM damu akina Dr. L***n*e, ambao watu walijua wapo na wana nia ya kukileta chama ipasavyo kwa kweli imewashangaza wapinzani wengi jinsi CDM ilivyoji- introduce venue, time not to mention a majority of the audience.

  Kuhusu CCM the word is Suzan Mzee keshaula (kwa mujibu wa CCM members) sasa hivi ni mshauri masaidizi wa waziri mkuu kuhusu mambo ya Diaspora na makazi yapo dar-es-salaam, utata sasa ni kumn'goa mwenyekiti kwa madai anakiua chama kwa maslahi binafsi.

  By the way tatizo letu watu tunaoishi afrika tunadhani kule ni kama huku watanzania ugenini hawana luxury ya kujiona kwamisingi ya dini ingawa kila mtu anaijua ya kwake kwa sababu wapo ugenini na ukimsikia mtu wa nyumbani ina kuweka at ease. Kwa hiyo kuna kueshimiana na kuelewana kwa hiyo it was common sense mkutano bar wakati wengine wapo kwenye saumu was bound not to attract many especially sehemu yenyewe imejaa waislamu, huyo Chris mwenyewe genge lake la karibu mostly ni waisalmu he should have known better.
   
 9. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hoja yako ni CV, unaweza kutueleza kuwa ina uhusiano gani na wewe 'kujiunga' na CDM?

  Nadhani una tatizo la akili ndogo kutawala akili kubwa. Nani alikuambia kila unaposikia neno 'PUB' basi unadhani wanauza vileo? Kuna Coffee pub kibao ulaya, lakini hata kama wanauza vileo ina maana hakuna kumbi za mikutano? Yawezekana hujawahi kutembea zaidi ya tz, hivyo neno pub kwa uelewa wa kibongo ni sehemu ndogo isiyo na hadhi. Magamba mmezoe ufujaji wa pesa na kujikweza kusiko na tija, jambo la muhimu hapa ni kukuza mtandao wa chama.
   
 10. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Olympic2012 nadhani hata huo uenyeketi unaoulilia ukatoswa huko UK hautusaidi..ningekuona wa maana ungekuwa unaulilia uenyekiti wa chama kata ya NAMANYERE s'wanga ungekijenga chama kwa walengwa.NADHANI UNA PROPOSAL uliyoandaa kupiga dil via iyo dhamana ukawashirikisha watu wakuwezeshe Ikawa patupu ukaumbuka..HAMIA MAGAMBA WANAWAHITAJI WATU KAMA NYIE
   
 11. Pangaea

  Pangaea JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana ndugu. Wewe kwako kuishi Ulaya ni kusoma sana? Hebu tupe CV yako tuione na tufahamishe ulishiri vipi kufanikisha uzinduzi wa tawi la CDM london?. Nikukumbushe tu kuwa uongozi ni kipaji na elimu ni "ingradient" tu ili kiongozi aweze kuwa na mtizamo sahihi. Unaweza kuwa na elimu kubwa sana lakini ukashindwa kuongoza hata familia yako.Mwisho Mbowe anatoka tena wapi? Kweli huoni kama uongozi wa CDM chini ya mbowe una mafanikio? Kama kweli wewe ni msomi hebu fanya tathmini.
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuna watu wamesoma lakini hawajaelimika, wapo wengi sana ndani na nje ya vyama vya siasa. Kitu muhimu ni uelewa wa maisha na jinsi ya kuyakabili. Chriss Lukosi pamoja na kwamba sijui elimu yake lakini ni mtu mwenye upeo mkubwa sana kimaisha. Ni mmoja kati ya vijana wachache sana wa kitanzania waliofanikiwa kimaisha London. Ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni (Serengeti Freight Forwarders) aka wazee wa kazi. Kampuni ambayo inasifika kwa kazi ya kusafirisha mizigo kwenda sehemu mbalimbali duniani. Ameweza kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania kwenye biashara zake London, na sasa ameamua kutumia uzoefu wake kukijenga na kukiimarisha Chadema London. Wewe unayedai CV ya Chriss Lukosi weka CV yako kwanza ama tuambie umefanya kipi katika maisha yako cha kujisaidia wewe mwenyewe.
   
 13. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Nilisema jana kwenye post moja na leo nitasema pia jamani tutofautishe pub ya bongo na pub ya duniani, Nasema tena Olympic2012 hayupo London na hajawahi hata kukanyaga ulaya, yeye atuambie kuhusu Kimboka au conner bar pale sinza. Sioni kama kunatatizo kwa CDM kufanyia mkutano huo bar
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Watoto waUK nyie wengi wenu tunawajua tabia zenu .Hebu tueleze sisi tuko Tanzania nawe uko UK na huyu jamaa tunawezaje kutoa CV .Kaomba nafasi nafasi Chadema Dar au wamejipanga wenyewe na kuanza mambo yao ? Acha upuuzi
   
 15. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa ukipewa hiyo CV itakusaidia nini? Mmekosa kazi ya kufanya mlichobakiza ni kuomba cv!!!!
   
 16. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Olympic 2012,

  Naona umelewa sana na upo chakari na operation Sangara na hii ya M4C. Ni utaratibu mzuri tu ambao unawakutanisha vijana woote ambao wanataka kubadilisha jinsi nchi yetu inavyoendeshwa kikoloni mamboleo ambapo sasa baadhi ya watanzania wanashirikiana na baadhi ya wasio watanzania kutorosha rasilimali zetu nje ya nchi.

  Ukoloni mamboleo ndio umewaweka CCM miaka 35 ya mtu mzima sasa ambae kama mtu umechezewa maisha yako, unajikuta huna nyumba, kazi nzuri ya maana na kila kukicha unadhulumiwa haki yako.

  Mkuu Olympic 2012, huitaji kumfahamu Chris Lukosi kwa namna hiyo, kwani yeye yupo mbali sana zaidi yako na huitaji kufahamu CV yake.

  Usilete personal issues na usitake kuharibu moto wa M4C.

  Watanzania wa Ulaya na Marekani na kwingine na hasa wa UK wana upeo wa aina yake, kwani ukiishi hapo UK na kufahamu utaratibu wa maisha ya kila siku na ukalinganisha na hapo unapoishi Tanzania unapata majibu mazito sana.

  Kwa kifupi watanzania walio nje na wale waliopo hapo TZ wenye kutaka mabadiliko ndio watakaobadilisha utaratibu mzima wa kuendesha nchi yetu na sio ninyi mliomo humo.

  Kwahio wewe subiri mabadiliko na ukiwa ni mmoja wa magamba inabidi ujiandae kupisha.
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  umeshasema mengi kuhusu huyo chris ukionyesha kwamba unamfahamu lakini hapo hapo unasema unataka cv yake, kwani cv ni kitu gani kwa akili yako?
  Pamoja na kuishi ulaya lakini mawazo yako hayana tofauti na mtu wa tandale kwa mtogole.
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Yanini mkatane vidole bure? Matawi yenyewe hata kwenye katiba ya chama hayatambuliki? Kimsingi hayo siyo matawi ila ni magenge ya washabiki. Huyo Dr. L***** anaweza na yeye kuanzisha genge lake, siyo lazima afuate genge la kina Chris.
   
 19. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ni katiba ya chama kipi unamaanisha magamba au?

  Halafu pili unadhani ni kwanini haya ni magenge na nini mwisho wake. Unaweza kuwa unapotosha watu hapa, au unataka kuwamaliza watu kihadhi na kisiasa.

  Tufafanulie maana tunajadiliana.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Fungua katiba ya CHADEMA sura ya saba 7.2.1, utagundua kuwa hayo yanayofunguliwa nje ya nchi ni magenge ya washabiki siyo matawi ya chama.
   
Loading...