Chozi Lisilofutika

Mambo sio mambo...

Asante Shunie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*CHOZI LISILOFUTIKA-05*
Mtunzi:Juma Hiza


Hakutaka kukata tamaa, aliendelea kumfuatilia huku hitaji lake kubwa likiwa ni kumueleza ukweli kuhusu hisia zake. Usumbufu uliendelea kuzidi zaidi na zaidi mpaka kikafikia kipindi kwa Suzani ikawa ni kero.

Hakutaka kuona akiendelea kusumbuliwa na mwanaume huyo hivyo alichoamua kukifanya ni kumwambia kwamba walitakiwa kwenda sehemu kwa ajili ya kuzungumza. Hilo halikuwa na tatizo hata kidogo, wakapanga mchana wa siku hiyo kwenda kwenye mgahawa wa Fresh coach.

Walipofika kwenye mgahawa huo wakaagiza chakula kisha wakaanza kuzungumza. Muda wote Revocatius alikuwa akitabasamu, aliamini ndoto yake ya kuwa na msichana huyo ilikuwa inakwenda kutimia.

“Kwanini umependa tuje sehemu hii na isiwe sehemu nyingine?” aliuliza Revocatius huku akitabasamu.
“Ni kwasababu ninamazungumzo muhimu na wewe,” alijibu Suzani huku mikononi akiwa ameshikilia uma na kisu tayari kwa kula chips kuku kwenye sahani aliyoagiza.

Revocatius alimtazama Suzani kwa macho ya huba, uzuri wa msichana huyo ulizidi kumchanganya vilivyo.

Mpaka kufikia hapo hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amekaa meza moja na msichana huyo tena walitakiwa wakizungumza kwa wakati huo.

Hilo hatuka kuamini, alihisi labda alikuwa katika ndoto lakini haikuwa hivyo. Aliendelea kumtazama Suzani huku moyo wake ukijawa na furaha isiyokuwa na kifani.

Siku hiyo Suzani alihitaji kuzungumza na Revocatius jambo moja muhimu. Lilikuwa ni kuhusu usumbufu wake, hakutaka kusumbuliwa na ndiyo sababu iliyompelekea akamuita sehemu hiyo ili amueleze na huo ndiyo uwe mwisho wa usumbufu kwani hakuhitaji kuwa naye.

Kwa upande wa Revocatius aliwaza tofauti na mawazo ya Suzani, alichoamini siku hiyo ndiyo siku ambayo alitakiwa kumueleza ukweli kwamba alimpenda na alimuhitaji katika maisha yake.

Kabla hajamueleza hilo, alihitaji kufahamu kitu kimoja ambacho kwa muda mrefu kilimchanganya na kumuumiza moyoni mwake tangu alipomfahamu.

“Kitu gani?” aliuliza Suzani huku akionekana kushangaa.
“Unanichukia?” aliuliza Revocatius.
“Siwezi kumchukia binadamu mwenzangu na kwanini nikuchukie kwani umenikosea kitu gani?” alijibu Suzani kisha akauliza swali.

“Nimehisi unanichukia ndiyo sababu nimekuuliza,” alijibu Revocatius.
“Hapana,” alisema Suzani.

Revocatius alipoambiwa hivyo akavuta pumzi na kutulia kwa kidogo, akaonekana akitafakari jambo fulani. Akaichukua glass ya juisi na kuanza kuinywa taratibu, alipotosheka akairudisha mezani halafu akainyoosha mikono yake yote miwili.

Muda huo alihitaji kushika mikono ya Suzani. Suzani akafanya kama alivyoombwa, viganja vyao vikakutana na kushikana huku sahani za vyakula na vinywaji vikiwa katikakati yao.
“Suzani,” alimuita huku akimtazama kwa macho ya huba.
“Abee,” aliitika.

“U msichana mrembo mno, una kila sifa ya kuwa msichana aliyekamilika. Hivi ni kitu gani ambacho umekikosa katika mwili wako? Jibu ni hapana. Embu angalia uzuri wako, mvuto wako, Mungu amekujaaliwa shepu ya kuvutia, angalia rangi ya ngozi yako nyororo, sauti yako yenye mvuto wa kimapenzi.

Kabla yako niliwahi kusikia watu wakisema kwamba wasichana wa kabila hasa lenu wachaga huwa hamnaga mvuto isipokuwa mmejikita zaidi kwenye utafutaji.

Tangu nikuone kwa mara ya kwanza umefanya nisiyaamini maneno hayo,” alisema Revocatius huku vigana vyake vikiwa bado vimeshikana na vya Suzani.

Alipoambiwa maneno hayo Suzani akavuta pumzi ndefu na kuziachia. Akatabasamu.

“Tazama hata tabasamu lako, linamvuto wa aina yake,” alisema Revocatius maneno yaliyomfanya Suzani kuanza kucheka.

“Asante kwa sifa zako,” alisema Suzani.
“Siyo sifa zangu hizi ni zako wewe.”
“Kwahiyo unataka kuniambia nini?”
“Ninakupenda Suzani, ninahitaji kuwa na wewe.”

“Hapana haiwezekani.”
“Kwanini?”
“Haiwezekani tu.”
“Unamaanisha nini?”
“Yaani sipo tayari kuwa na mwanaume kwasasa,” alijibu Suzani.

Revocatius hakutaka kuamini kama kweli alimkosa msichana huyo tena katika mazingira hayo ambapo palikuwa na uwezekano mkubwa wa kumpata lakini ilishindikana.

Suzani alimaanisha kile alichokuwa akikizungumza, hakutaka kuishia kumwambia kwamba hakuhitaji mwanaume tu bali aliendelea kumwambia kwamba alitakiwa kusoma na kuyaacha mapenzi kwani hayakuwa sababu iliyompeleka chuo kusoma.

Hakutaka kupoteza muda wake, alipomaliza kuyazungumza hayo aliinuka na kuanza kuondoka eneo hilo huku akimuacha Revocatius akiwa bado amekaa.

Siku hiyo kwa upande wa Revocatius ilikuwa ni siku ya maumivu, hakuamini kama msichana huyo alimuacha katika mazingira yale huku akiwa amemuambia maneno makali kiasi kile.

Mawazo yalimzonga kichwani kiasi kwamba mpaka akashindwa kuendelea kula, alichokifanya akalipa bili ya chakula na kisha haraka sana akaanza kumkimbilia Suzani. Alipofika nje ya mgahawa huo hakumuona, akazidi kuchanganyikiwa.
****
Urafiki kati ya Suzani na Enock uliendelea, kutoka Facebook ambapo waliishia kuchati na sasa walifikia kubadilishana namba za simu, wakawa wanapigiana simu na hata wakati mwingine kupigiana kwa njia ya video call, WhatsApp.

Suzani alijisikia furaha sana kuwa na urafiki na mwanaume huyo ambaye alikuwa akiishi Mwanza.

Alionekana kuwa mcheshi, aliyefahamu mambo mengi sana kuhusu dunia lakini pia alikuwa na hofu ya Mungu.

Sifa za mwanaume huyo zilimchanganya sana Suzani, kila siku hakuacha kuwasiliana naye huku muda mwingi alipokuwa peke yake kichwa chake kilikuwa kikimuwaza mno.

Baada ya kupita wiki mbili Enock uvumilivu ulimshinda, akaamua kumueleza ukweli Suzani kwamba alimpenda. Tofauti na ilivyokuwa kwa wanaume wengine, Suzani akakubali kuwa na mwanaume huyo ambaye alimuona kuwa ni mtu sahihi. Alichokiamini ni kwamba Mungu alimleta katika maisha yake kupitia mtandao huo wa kijamii wa Facebook.
Siku zikaendelea kukatika huku wawili hao wakiwa tayari ni wapenzi.

Wakaonekana kuhitaji kuonana, kwa upande wa Suzani ilikuwa ni vigumu kufunga safari mpaka Mwanza kumfuata mwanaume huyo hivyo alichoamua kukifanya ni kumwambia Enock kwamba alitakiwa kumfuata Kilimanjaro, Moshi mjini.

Hilo halikuwa tatizo hata kidogo. Enock alikubali na baada ya kupita siku tano akafunga safari mpaka Moshi mjini. Alipofika akachukua chumba katika hoteli ya nyota tatu ya Osy Grand iliyokuwepo mtaa wa riadha.

Alikumbuka kumwambia Suzani kwamba alifika Moshi mjini na kwa wakati huo alikuwa hotelini. Suzani hakutaka kuamini kama mwanaume huyo ambaye alikutana naye Facebook mpaka kufikia hatua wakaanzisha mahusiano ya kimapenzi alikuwa amemfuata Moshi kama alivyomwambia. Hilo lilimfurahisha mno, muda wote alikuwa haamini.

Kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha kukaribia kufanya mitihani ya Mid semister ya chuo na aliomba ruhusa nyumbani kwamba angekaa hostel kwa muda wa mwezi mzima kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo hivyo hakukuwa na tatizo la yeye kwenda kukutana na mwanaume huyo kwenye hoteli hiyo ya Osy Grand.

Kutoka chuo cha ushirika mpaka kufika mtaa wa riadha ambapo ilikuwa hoteli hiyo hakukuwa kuna umbali mrefu sana kwa usafiri wa kawaida kama hiace, lakini kutokana na hamu kubwa aliyokuwa nayo Suzani ya kumuona mwanaume huyo, aliamua kuchukua bajaji ambayo ilimfikisha haraka mpaka ilipokuwa hoteli hiyo.

Alipofika hotelini hapo alimpigia simu Enock na kumwambia kwamba alikuwa nje ya hoteli hiyo. Baada ya dakika chache Enock alitoka nje na macho yake kukutana na macho ya Suzani. Kwa furaha Suzani akamkimbilia Enock kisha wakakumbatiana.

*Je, nini kitaendelea?*
*Huu ndiyo mwanzo wa kisa cha Suzani kupata ujauzito mpaka kutelekezwa na kufukuzwa nyumbani kwao.*

*Endeleakuifuatilia simulizi hii yenye kuumiza na kutia moyo wa waliyokata tamaa.*
 
Tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli mapenzi hayana mwenyewe....!!!

#Acha nilie tu, i think ni zamu yangu ya kulia.....
#Ahsante aunty Shunie

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…