Chozi Lisilofutika

Asante shunie. Nimekumbuka enzi za shule ya sec.mpaka namaliza siijui sausage .kuna mtu aliniambia ndege mzuri hunasa kwenye tundu bovu. Ile kukaa nyumbani kusubiri majibu nikaangukia kwa bad boy player hatari. Mengine bora nijinyamazie tu
 
Asante shunie. Nimekumbuka enzi za shule ya sec.mpaka namaliza siijui sausage .kuna mtu aliniambia ndege mzuri hunasa kwenye tundu bovu. Ile kukaa nyumbani kusubiri majibu nikaangukia kwa bad boy player hatari. Mengine bora nijinyamazie tu
Ebu malizia bwana
 
*CHOZI LISILOFUTIKA-03*
Mtunzi:Juma Hiza

Revocatius hakutaka kuamini kama ule ndiyo ulikuwa mwisho wa kuzungumza na Suzani.

Kwa dakika kadhaa alizozungumza naye tayari moyo wake uliingiwa na hisia za kimapenzi. Alihitaji kumuelezea ukweli wa hisia hizo lakini alipoyakumbuka yale majibu ya mkato alisita kufanya hivyo.

Kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo ambavyo moyo wake ulizidi kujawa na mapenzi kwa msichana huyo. Hakutaka kuficha hisia zake, aliamua kuwaeleza marafiki zake Hiza na Fredy juu ya hisia hizo.

Walipoambiwa hayo Hiza na Fredy hawakuta kumficha kitu, walimueleza ukweli kwamba msichana huyo hakuwa rahisi kama alivyokuwa akidhania. Mpaka kufikia muda huo alisumbuliwa na wavulana wengi na wote hakuna aliyefanikiwa kumpata.

“Hilo sijali, nataka ajue ukweli kwamba nampenda tu,” alisema Revocatius huku uso wake ukionekana kumaanisha kile alichokuwa akikizungumza.

Haraka sana hakutaka kupoteza muda, akaanza kumfuatilia msichana huyo. Alichokuwa akihitaji kwa wakati huo ni kumueleza ukweli kuhusu hisia zake ambazo zilianza kumuumiza.

“Samahani tunaweza kuzungumza?” aliuliza Revocatius huku akimtazama Suzani, wakati huo alikuwa kantini akila pamoja na marafiki zake.

“Huoni nakula jamani,” alijibu Suzani kwa sauti ya kulalamika.
“Ukimaliza.”
“Hapana sina muda huo.”
“Kwanini?”

“Nipo bize labda siku nyingine.”
“Okay basi naomba unipe namba yako ya simu ili nikutafute.”
“Siwezi kuitoa,” alijibu Suzani na kufanya marafiki zake wamshangae.

Kila mtu alihisi labda alifanya utani na kwamba angempa namba ya simu mvulana huyo aliyesimama mbele yao lakini haikuwa hivyo, kile alichokijibu ndicho alichokimaanisha.
****

Revocatius alipokuwa nyumbani kwao, akili yake ilimfikiria msichana huyo kupita kawaida.

Hakujua ni njia ipi alitakiwa kuitumia kumpata msichana huyo. Kila njia aliyoitumia ilishindikana na kibaya zaidi ni kwamba hata nafasi ya kuzungumza naye aliikosa. Hilo likazidi kumuumiza mno.

Dadika kadhaa alizokaa chumbani kwake huku akiwaza na kuwazua ni nini alichotakiwa kukifanya kwa msichana huyo, akapata wazo. Lilikuwa ni wazo la kutafuta namba yake ya simu.

Alichokiamini ni kwamba kama angefanikiwa kuipata namba ya simu ya msichana huyo kazi iliyokuwa imebaki ni kitendo cha kumpigia simu na kumueleza ukweli wa hisia zake, hata kama angemtukana lakini angekuwwa tayari amezungumza naye na kumueleza ukweli.

Kwa wakati huo aliwaza ni nani ambaye angeweza kuwa na namba ya simu ya msichana huyo.

Haraka sana akampigia simu rafiki yake Hiza, akumuomba namba ya simu ya Suzani. Alichojibu Hiza ni kwamba hakuwa na namba zake za msichana huyo lakini pia alimwambia kuwa Fredy na yeye asingeweza kuwa nazo.

“Ila nimepata wazo,” alisema Hiza.
“Wazo gani?”
“Wale marafiki zake hawawezi kukosa. Ukiwatumia wale vizuri lazima utaipata,” alisema Hiza.

Alichokizungumza Hiza kilikuwa ni kweli kabisa. Kama Revocatius alihitaji na namba ya Suzani basi alitakiwa kuwatumia marafiki zake kwani wasingeweza kuikosa.

Siku iliyofuata haraka sana hakutaka kupoteza muda, alimtafuta mmoja kati ya marafiki zake Suzani aliyejulikana kwa jina la Rukia.

Akamueleza shida yake kubwa ilikuwa ni namba ya simu ya Suzani. Rukia alishtuka baada ya kusikia hivyo, hakuwa tayari kuitoa namba ya simu.

“Hapana sina nia mbaya, nimekosa muda wa kuzungumza naye na ndiyo maana nimekuomba unipe namba yake ili nimpigie,” alisema Revocatius.

“Akijua nimekupa mimi itakuwa tatizo kwa upande wangu lakini.”

“Nakuahidi sitamwambia, shida yangu nataka kuzungumza naye,” alisema Revocatius huku akionekana kuwa na uhitaji mkubwa na namba hiyo.

Baada ya mazungumzo hayo Rukia alikubali kuitoa namba ya simu ya Suzani. Revocatius hakutaka kuamini kama alifanikiwa kuipata namba ya simu ya msichana huyo.

Hakutaka kupoteza muda, akamtumia ujumbe mfupi wa salamu na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuchati kwao.
“Safi nani wewe?” alijibu Suzani.

“Kisoka.”
“Yupi?”
“Revocatius?”
“Ndiyo yupi?”
“Mara ya mwisho tulikutana pale kantini nikaomba kuzungumza na wewe lakini ikashindikana.”

“Ooh! Nimekufahamu, namba yangu umeipata wapi?”
“Kwani kuna ubaya mimi kuwa na namba yako jamani?”

“Ndiyo tena sana.”
“Kwanini sasa?”
“Basi tu.”
“Nikuulize?”
“Uliza.”
“Hivi kwanini unanichukia, hutaki kabisa kuzungumza na mimi?”

“Sipendi tu.”
“Uko wapi?” aliuliza Revocatius kwenye ujumbe lakini haukujibiwa. Alihisi labda ujumbe huo haukufika hivyo akarudia kuutuma tena lakini haukuweza kujibiwa. Ukimya huo ukazidi kumchanganya na kumuumiza.

****
Katika kipindi chote hicho ambapo masomo yaliendelea chuoni hapo, tabia ya Suzani ilionekana kuwa tofauti na tabia za wasichana wengine.

Hakuwa ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa kwa marafiki zake ambao walikuwa na akaunti Facebook pamoja na mitandao mingine ya kijamii.

Hilo liliwashangaza sana marafiki zake, walipomuuliza aliwajibu kwamba hakujisikia kujiunga na mitandao hiyo.

*Je, nini kiliendelea?*
*Tukutane Kesho.*
 
*CHOZI LISILOFUTIKA-04*
Mtunzi:Juma Hiza

Walipoambiwa hivyo hawakutaka kuamini, walihisi labda walidanganywa. Walichokifanya wakachukua simu zao, wakaingia Facebook kisha wakaanza kulitafuta jina la Suzani Mushi.

Yakatokea majina ya Suzani kama kumi, wakaanza kupitia akaunti moja baada ya nyingine. Kila picha ya Suzani waliyekuwa wakimuangalia, hakuwa Suzani yule waliyemfahamu. Hilo likazidi kuwachanganya.

Hawakutaka Suzani aendelee kuishi maisha ya kizamani kwani kwa kipindi hicho dunia ilikuwa tayari imetawaliwa na utandawazi.

Licha ya kwamba msichana huyo alilelewa katika mazingira ya kidini na wazazi wake yaliyomfanya mpaka ashindwe kuwa bize na mtandao huo, hata pale alipoenda kufanya ibada kwenye kanisa la Seventh Day Adventist, mchungaji wa kanisa hilo alikuwa akisema kwamba shetani alikuwa akifanya kazi yake katika mtandao wa facebook kwa ajili ya kuwapotosha watu ili wasahau kufanya ibada.

Hilo hawakutaka kukubaliana nalo, walichoamua kukifanya wakaanza kumshawishi ajiunge na mtandao huo kwani kuna mengi mazuri yalikuwa yakimpita.

“Watu wamepata wapenzi, kazi, marafiki kwenye mtandao huu,” alisema Brenda rafiki yake Suzani.

“Kama mimi facebook imenikutanisha na marafiki wengi sana ambao sikuwahi kuwaza kama kuna siku ningewafahamu,” alisema Rukia huku akiendelea kuusifia mtandao huo.

Kwa jinsi Brenda na Rukia walivyokuwa wakiusifia mtandao huo wa Facebook, Suzani akajikuta akitamani na yeye kufungua akaunti katika mtandao huo. Hilo wala halikuwa tatizo hata kidogo, akafanikiwa kufungua akaunti.

Moyo wake ulikuwa ni wenye furaha baada ya kuwa na akaunti facebook. Akaanza kupost picha zake huku kila siku akizidi kupata idadi kubwa ya marafiki.

Wanaume wengi waliyokuwa watumiaji wazuri wa facebook walipoziona picha zake walizipenda na kumtamani hivyo wakaanza kumsumbua kwa kumtumia ujumbe inbox. Kila ujumbe aliyotumiwa ulikuwa ni wa mapenzi na kila mwanaume alitamani kuwa naye.

Picha zake zikazidi kuwachanganya wanaume wa facebook. Humo kulikuwa kuna wazungu, waarabu, wachina na wanaume kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao walitokea kuvutiwa naye.

Hakukuwa kuna mwanaume aliyeziona picha za msichana huyo kisha asiache kuingia katika akaunti yake ili aendelee kuzitazama picha zake nyingine zaidi na zaidi.

Suzani alikuwa na mvuto na hii ndiyo sababu ambayo ilipelekea kila mwanaume aliyemuona akamtamani na kuanza kumsumbua.

“I need to talk with you,” (Ninahitaji kuzungumza na wewe) ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa mzungu mmoja facebook aliyekuwa akitumia jina la Kenedy.
“I love you Suzani,” (Nakupenda Suzani) alituma mzungu mwingine.

Kipindi hicho Suzani kila alipokuwa akiingia facebook, alikutana na meseji nyingi ambazo alitumiwa na wanaume tofautitofauti. Kila mwanaume alisema anampenda na hivyo kutaka kumuoa.

Hakukuwa kuna mwanaume aliyepata nafasi ya kuchati ama kuzungumza na msichana huyo kwani hata pale walipokuwa wakimtumia ujumbe, haukuweza kujibiwa, Suzani alikuwa akiusoma na kuachana nao.

Akazidi kuonekana kuwa msichana wa gharama, thamani yake ikazidi kupanda siku hadi siku.

Sio chuoni tu bali hata wanaume waliyokuwa wakimuona Facebook walizidi kuchanganyikiwa.
Siku ziliendelea kukatika, Suzani akaanza kuonekana akiutumia muda wake mwingi kuperuzi Facebook.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kila kitu. Akazidi kuwa mtumiaji mzuri wa facebook mpaka pale alipoanzisha urafiki na mwanaume mmoja kwenye mtandao huo aliyejulikana kwa jina la Enock Mabula.

Huyu Enock alimsumbua sana, kila siku kazi yake kubwa alikuwa akimtumia ujumbe Suzani lakini haukuwa ukijibiwa. Hilo lilimsononesha mno na kumfanya kuanza kukata tamaa.

Siku moja Suzani alipost picha yake facebook akiwa maeno ya chuo, akaandika kwamba hakuwa sawa siku hiyo hivyo alihitaji marafiki wa facebook ambao wangeweza kumfariji mpaka arudi katika hali yake ya kawaida.

Siku hiyo Enock alipoiona post ya msichana huyo kwa kuwa mara kwa mara alikuwa akiingia facebook na kumuangalia, haraka sana akakumbuka kulike na kucomment kwa kumpa pole na kumsifia lakini pia hakuishia hapo, akamtumia ujumbe.

Baada ya kupita dakika moja ujumbe huo ukajibiwa. Enock hakutaka kuamini kama msichana huyo aliweza kumjibu ujumbe wake kwani kabla ya hapo aliwahi kumtumia ujumbe zaidi ya mara tano tena katika siku tofauti tofauti lakini hakuwahi kujibiwa hata mara moja.

Siku hiyo ikawa ni siku yenye furaha kwa upande wake, akaurudia kuusoma ujumbe huo mara mbilimbili huku akiwa haamini kabisa. Hakutaka kupoteza muda na yeye akaujibu na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuchati kwao.

Walichati sana siku hiyo mpaka kufikia hatua wakabadilishana namba za simu. Enock alifurahi sana, hakutaka kuamini kama aliweza kuchati siku hiyo na msichana huyo mpaka kufikia hatua ya kupewa namba ya simu.
****
Revocatius mapenzi yaliendelea kumtesa moyoni mwake, kila alipomuona Suzani alizidi kuchanganyikiwa. Alimpenda sana lakini msichana huyo hakuonekana kujali kitu.

Alimpigia sana simu, alimtumia kila aina ya ujumbe msichana huyo lakini majibu aliyokuwa akijibiwa yalizidi kumuumiza. Hakujua kama kipindi hicho ambapo alikuwa akimfuatilia tayari alishakuwa na ukaribu na Enock mwanaume ambaye alimpatia Facebook.

Je, nini kitaendelea?
 
😢😢
 
narudi,naweka alama
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…