Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,410
- 38,702
Nimejaribu kuwaza kama Chozi la Mzee Mizengo Kayanza Pinda alilolitoa Pale Bungeni akiwa Waziri Mkuu wakati akizingumzia Mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa Ngozi, al maarufu kama Albino, Kama lilileta manufaa yaliyokusudiwa. mbali ya kukisia tu hisia zake zilikuwaje kwa kweli hakuna mpaka leo aliyewahi kumuuliza ilikuwaje mpaka chozi likammwagika mbele ya Kadamnasi ile na wakati taifa zima likimtizama kupitia Luningani!
Lakini tena wakati wa kumtangaza Mgombea Urais kupitia CCM Pale kwenye Ukumbi wa mikutano wa CCM mjini Dodoma, Pinda alimwaga tena chozi. Kama ilivyokuwa mwanzo hakuna aliyewahi kumuuliza mfuga nyuki huyu maarufu kama ni nini hasa kilimsibu hadi tena machozi yakamwagika.
Kama Pinda alikuwa anasikitika kwa kauli yake kwamba wanaouwa Maalbino nao pia wauawe, mbona tena mbele ya safari akatoa kauli yenye utata ya "wapigwe tu"? Chozi lake la Pale bungeni halikumsaidia kubadili mtazamo dhidi ya watu wanaotenda uhalifu? Kauli zake hizo hazikuacha athari ambazo baadhi ya watu wanaathirika kwa kuwa yeye mwenyewe hajawahi kuzikanusha kindakindaki kwamba si mtizamo wake bali labda maneno yalimteleza?
Lakini kwa sababu hakuna waliowahi kumuuliza Pinda ni kwa nini huwa anamwaga chozi kwenye matukio yenye mbinyo wa hisia, mpaka leo Chozi lake wakati Magufuli anatangazwa kuwa Mgombea wa Urais kupitia CCM bado halijapata tafsiri. Pinda aliona amedhulumiwa? Au alisononeshwa na kuchaguliwa kwa aliyekuwa Waziri chini yake kuwa Mgombea wa nafasi hiyo nyeti kwenye taifa letu?
Najiuliza chozi la Pinda lilibadili hali ya mambo ili Maalibino wasiuawe, au chozi lake mwana wa Mkulima wakati Magufuli anatangazwa kuwa mgombea lilibadili mtizamo wake dhidi ya chama chake? Au lilikuwa ni chozi tu lisilo na taathira?