WanaJF!
Kwa utafiti nilioufanya kutoka kwenye mamlaka mbalimbali za vyombo vya anga, nimegundua kuwa chombo kama helikopta au maarufu kama "chopa", hutumia si chini ya dola za kimarekani (3000 - 3500) kwa dk 45 angani, na pesa hizo ni sawa na Tshs. 5,700,000 kwa exchange rate ya (1 USD = Tshs 1630).
Baada ya mchanganuo huo wa kimahesabu, nikasema ngoja nitazame kiasi cha fedha ambacho CHADEMA wametumia kama gharama za kupaa na "chopa" katika mikoa tisa (9) hapa nchi kwenye shughuli zao za ukusanyaji wa maoni.
Ikiwa kutoka Dar mpaka Morogoro ina gharimu kiasi cha Tshs 5700000 (Dar mpaka Moro kwa helikopta ni saa 1 tu), hivyo kuzunguka mikoa tisa (9) Tanzania (tufanye masaa 20) ukiwa angani sio chini ya Tshs. 115,000,000.
Kiasi cha Tshs 115,000,000 ni gharama ya usafiri tu kwa makadilio ya chini, bado posho, vyakula na vinywaji, na kwa kuwa CHADEMA ilikuwa na timu kubwa kwenye shughuli hii, hivyo gharama zote zinaweza kwenda mpaka Tshs. 150,000,000.
Aidha, jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba CHADEMA ilipewa ONYO na tume kuwa utaratibu wa kukusanya maoni haufanywi kwa kuendesha mikutano ya hadhara, matokeo yake baada ya CHADEMA kukaidi maelekezo hayo (kwa kuwa waliona kama watakosa POSHO) hivyo tume imegoma kupokea maoni yao.
Je, nini faida ya matumizi ya pesa zote hizi?

HAMY-D,
Kama nilivyosema siku zote, aidha tatizo ni elimu, uelewa mdogo au kukosa tu umakini na kukurupuka.
Napenda kufafanua kwa manufaa ya Watanzania,na labda wewe pia Kama itakusaidia:
1. Chadema haijapewa ONYO lolote kama unavyotaka kuwaambia Watanzania. Kama kungelikuwa na Onyo lolote lingelifika Ofisini kwa Katibu Mkuu, na Ofisini kwangu hadi ninapokujibu hakuna barua yeyote ya Onyo kwa Chadema Kama unavyotaka kuonyesha. Inawezekana unaleta majungu ya mitaani na kutaka kuyahalalisha.
2. Ni vizuri watanzania wakaelewa. Kukusanya maoni ni lazima uende kwa watu, huwezi kukusanya umekaa mezani, au labda uwe unapika matokeo mezani. Hivyo, au ni lazima utatembea kwa miguu, utapanda baiskeli, au gari au Chopper Kama Chadema tulivyofanya. Njia utakayotumia ndiyo itakayokupatia matokea. Ni dhahiri ulienda kwa miguu utawafikia watu wachache zaidi na maeneo ya Karibu tu. Chadema, Timu ya Taifa tu tulifika Majimbo 81 ambako tulipata maoni toka kwa Watanzania 3,200,000 kwa Timu zote mbili ( na siyo Mikoa 9 tu Kama unavyosema. 9 ni mikoa aliyofika Katibu Mkuu tu, inawezekana hesabu pia imekupiga chenga. Hiyo ndiyo Takwimu sahihi kutoka kwa mamlaka husika hivyo usipige ramli wakati tulioyatekeleza tuko kukufafanulia). Tofauti ikon dhahiri kabisa Kati ya waliotumia Chopper na waliotumia njia nyingine.
3.Aidha, Kama umesoma vizuri, "maoni" yaliyokuwa yamewasilishwa kwa njia ya Randama yenye vipengele 66 yalipokelewa na Tume( bahati mbaya Waandishi wa Habari walizuiliwa kuingia ukumbininkwa utaratibu wa Tume. Lakini picha ziko ukitaka kuziona wakatimTunakabidhi. Kitu ambacho hakikupokelewa, na wala siyo " kukataliwa" Kama unavyotaka kusema au baadhi ya vyombo vilivyoandika.Tume " Haikujipanga vizuri" kupokea vielelezo ya jinsi Taasisi husika ilivyokusanya maoni kutoka kwa Watu. Ndiyo maana ukitaka kujua kweli Kama hayo maoni yametokana na wananchi utathibitisha vipi, Kama katika utaratibu wako huna utaratibu wa kupokea vielelezo. Ndiyo maana tukatoa tahadhari matokeo yasije yakChakachuliwa kwa watu kuyatengeneza tu mezani. Chadema tulitumia njia za kisayansi a) mabaraza ya wazi ambako kwenye kila fomu inaonyesha jina la mtoa pendekezo, jinsi yake, namba yake ya simu na mkoa,Wilaya au Jimbo au Kata anakotoka. b) njia ya pili ni kupitia na. Maalum ya Simu na tumeweka print out ya maoni yote ya SMS zilizopokelewa na mtambo maalum wa Computer iliyokuwa inapokea SMS hizo, c) kupitia email address iliyoanzishwa kwa lengo hilo tu, yaani Chademamaoni@gmail.com na hatimaye kupitia mitandao ya Jamii ikiwemo JF na FB na tunaw ashukuru waendesha mitandao yote hiyo kwa kazi nzuri iliyonywa na mitandao Yao.
4. Kama unajua maoni ya Chadema yalikusanywa chini Sheria ya Marekebisho ya Katiba, Kif. 18(6) na miongozo iliyotolewa na Tume kufanya kipengele hicho kutumika, Warioba na au Tume kwa ujumla wake, haiku juu ya Sheria. Wanachopaswa kufanya ni kutii Sheria, na kwa mujibu wa Sheria hawana "Hiari ya Kupokea au Kukataa kupokea maoni yanayowasilishwa kwa mujibu wa Sheria". Ndiyo maana Maoni yalipokelewa kupitia " Randama" na Kiambatanisho A ambacho kilihusu kwa upon sana maelezo ya Kwanini "Serikali 3 na siyo 2". Hivyo, WanaJF na Watanzania kwa ujumla muwe na Amani. Maoni yamepokelewa Kama tulivyoyawasilisha, isipokuwa tu tulilalalamika, Tume kutopanga na kuchukulia zoezi la kura ya Maoni ya Katiba Kama jambo la Kawaida tu. Kwa yeyote anayetaka kuona Kama yalipokelewa afire ofisini tumwonyeshe Nakala ya Ofisi iliyogongwa muhuri wa Tume na picha za makabidhiano zilixopigwa na Maofisa wa Chama.
Hujatoa chanzo cha gharama ulizotuwekea hapa.
Nashangaa wana jamvi, tunaojiita Great thinkers tunachangia tu bila kuhakiki kwanza ukweli wa data zilizowekwa mbele yetu
Data ulizotoa juu ya gharama ni za UONGO, tena wa makusudi ili kupotosha!
Gharama ulizotupa ni za kuendesha madege makubwa kama Boeing 777, au Airbus A330-200, ambazo hubeba abiria zaidi ya 300.
Mchanganuo sahihi ni huu hapa, na source za habari zinajieleza!!!
![]()
Hiyo gharama ni $1.16 per mile, ambayo inaifanya iwe chini ya $1 kwa kilometre!
Ukipenda kuchukua gharama kwa saa nazo data zake ni hizi hapa:
![]()
$262.47 kwa saa kwa hiyo Enstrom na ile ye Robinson ni $ 229 kwa saa!
Hivi UONGO, imekuwa sera rasmi ya propaganda za CCM?