MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,242
- 43,793
CHONDECHONDE VIONGOZI WA SERIKALI YA CCM, MUWE NA MAELEWANO.
Natumaini wanaJF mko wazima kabisa.
Leo baada ya wengi wenu kunipigia simu na kunisihi niseme neno kuhusu haya mambo ya viongozi wa serikali wanaotokana na Chama kilichobeba matumaini ya watanzania, CCM, kukwaruzana wao kwa wao kama vile ilivyo upinzani na CCM. Kiukweli matukio yapo na hayahitaji uelewa mkubwa kuona watu hawako kitu kimoja. Kwa mfano kuna clip inaenea mitandaoni ya mabishano kikaoni kati meya wa Kinondoni na mkurugenzi wake, kule Arusha nako mbunge alinukuliwa akimlaumu Mkurugenzi na kuna clip ikimuonesha akipinga baadhi ya maelekezo ya mkurugenzi kwa wafanyabiashara. Hiyo ni mifano miwili ya wazi. Bungeni nako ilibidi Rais Samia aingilie kati na kutaka wabunge wajadili mambo ya muhimu.
Ninachoweza sema ni kwamba baadhi ya viongozi hawana sifa za kutosha kuwa kwenye nafasi walizopo ila kwa nguvu ya Chama Cha Mapinduzi na Hayati Mwendazake wakaweza kupenya hadi kukalia viti walivyokalia. Kwangu mimi sio tatizo na ni kawaida kwenye kutafuta riziki. Matarajio yalikuwa kwamba baada ya kupata nafasi basi hata kama ulibebwa inabidi kujitutumua na kuonyesha kuwa ulistahili.
Madhara ya haya mambo ni nini? Ni kutengeneza mpasuko kwenye chama kilichobeba matumaini ya watanzania, CCM. Pia kuleta ugumu kwenye utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi. Ikumbukwe hadi sasa hakuna chama mbadala wa CCM ndo maana CCM bado inapendwa na kuaminika na watanzania wote. Baba wa taifa alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM lakini sisi wanachama wazalendo hatutakubali huo upinzani uje kwa staili hii ya watu wachache kuvuruga. Ilani ya CCM inahitaji miaka mingi sana ijayo ili kuivusha Tanzania hadi uchumi wa juu kabisa. Bado ni mapema sana kwa CCM kugawanyika.
Nashauri viongozi wa CCM wakemee hawa viongozi wasioelewana kazini. Vinginevyo wananchi watatuadhibu kwa kutunyima kura kwenye uchaguzi ujao. Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Mungu ibariki CCM! Mungu ibariki Tanzania.