Dangire
JF-Expert Member
- Oct 5, 2011
- 221
- 68
Nchi hii ni yetu sote watanzania. yaliyotokea katika siku za hivi karibuni, na yanayoendelea kutokea (huko masasi) si dalili njema hata kidogo kwa amani ya nchi yetu. ikumbukwe kuwa, 'hata mbuyu ulianza kama mchicha'. Toka mwaka jana zilipoibuka chokochoko za kidini (eg. kuchoma makanisa, nk.) haikuwa dalili njema.
Kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi si UUNGWANA. haileti picha njema kwa nchi yetu na ktk uso wa dunia pia. mbona tunajiandalia maangamizi yetu wenyewe? Si busars, si sahihi, tuache ghasia hizi.ni kipi kisichozungumzika?
Kwa serikali. haiingii akilini kuona serikali ikishindwa kushughulikia 'sintofahamu' zinazojitokeza nchini. hivi ni mpaka waleta 'ghasia' hawa watakapovamia ikulu ndio serikali ijue kuwa hatupo salama? iko hivi...kwa sasa chokochoko yaweza kuwa 'gesi ya mtwara'. ila wanaopambana utakuta ni watu tu ambao kwa muda mrefu walikuwa tu wanatafuta nafasi (opportunity) ya kutekeleza adhma yao...waganga njaa, wadini, 'wakabila' washirikina, nk. waweza kuona kuwa huu ndio wakati! hivyo ni hatari kumbwa kushindwa kuzima ghasia hizi kwa haraka. hivi ikiwa wanachi wana hoja, serikali inashindwa nini kukaa nao na kupata suluhu?
hivi, ndio tuseme kuwa ccm na serikali kwa ujumla mmeshindwa kuongoza nchi? kama ndivyo, mnasubiri nini magogoni?
...inatia hasira na uchungu kweli.
nawasilisha.