Chonde chonde ndugu zanguni naombeni msaada wenu. Nina wakati wa kuhuzunisha moyo

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,514
Katika shemeji zenu wavumilivu huyu ni mvumilivu sana. Mpaka naogopa na kumwonea huruma sababu ni mwanamke mzuri anayejielewa ila kanipenda mimi mtu wa hovyo kabisa. Nisiyemfaa, mjinga, bwege na fala.

Hili jambo limenitesa sana moyo wangu.mdada ameshawahi nifumania mara 2 akanisamehe na kunambia nakosa nini kwake.nijitahidi kuachana na tabia mbaya ambazo hazitanisaidia kitu.

Sasa sina kazi muda flani. She is the one anayeniwekea mafuta kwenye gari na kuhakikisha tunasimamisha shughuli za kiuchumi.

Jumamosi shemeji yenu ana birthday. Mwenzenu sina hata 1000 mfukoni. Chonde chonde ndugu zanguni mnichangie nimtoe out shemeji yenu. Au hata nimnunulie zawadi.

Nawaombeni sana wana JF mnipige tough ktk hili sisi wanaume huwa tunabebana kuokoa jahazi.jahazi langu linazama. Nahuzunika birthday yangu she did a lot. Alitumia almost tsh 550,000 for me. Mimi nahitaj hata 100,000 tu.

Naahidi kuwa baada ya sherehe ntamwambia yote nliyoyafanya ni kwa hisani ya watu wa JF. Afahamu undugu si kufanana.ni kufaana nanyi mkinifaa kwa jua nami ntawafaa kwa mvua.
 
Mimi ingekuwa shida nyingine ningekuchangia ila kama shida yako ndiyo hiyo bora nichangie wengine wanaohitaji matibabu na ada, maana mimi mwenyewe hata bday yangu uwa inaweza kupita bila kuikumbuka hadi nikumbushwe, ninachoumbuka ni bday ya mwanangu tu.
Siku ukiumwa ukataka mchango count me in.
 
Vipi hawa dada zako washaolewa?

 
Back
Top Bottom