Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 38,611
- 49,009
Kwa hali hii ya vugu vugu la hamaki kwa baadhi ya watia nia kuhama baada ya kukatwa.
Ingawa hakuna dalili ya ushindi kwa namna yoyote ile....
Uelekeo baada ya kuhama na kushindwa katika uwanja wa ushindani ni kwa wahusika kuelekeza nguvu zao msituni.
Dalili za kushindwa zipo kwa viashiria vya kuonesha azma ya wazi kabisa ya ung'an'ganizi, uliowashtua wengi.
Kila mwenye akili zake anauliza, huko kuna nini mpaka nguvu zote hizo zitumike....
Si ajabu sana, hata baada ya nafasi kupatikana kwa kushindana na waliowakata, endapo wakishindwa kugeuza uhasama wa moja kwa moja.
Ni rai yetu sisi kina kamchape, ambao hatujui sababu za kukatana, na kwanini kina flani wakahama, kuachiwa amani yetu ambayo ndio zawadi pekee tuliyobakiwa nayo baada ya rasilimali zetu kuendelea kuwanufaisha wachache.
Mnaposuguana, msituharibie vimkate vyetu. Bado tunahitaji amani....
Hatutawaunga mkono mkitaka kwenda msituni...