‘Chokochoko dhidi ya Bunge ni uchochezi’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Chokochoko dhidi ya Bunge ni uchochezi’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 22, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  ‘Chokochoko dhidi ya Bunge ni uchochezi'
  Imeandikwa na Stella Nyemenohi; Tarehe: 21st February 2010 @ 23:55
  HabariLeo


  MABALOZI wa amani waliounda umoja ujulikanao kama Amani Forum wamewakosoa wanaharakati wanaoandaa maandamano dhidi ya Bunge kwa kusema kitendo hicho ni choko choko zinazoashiria uvunjifu wa amani unaofanywa na watu
  wenye maslahi binafsi.

  Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema ambaye ni mmoja wa wajumbe pamoja na Katibu wa Umoja huo, Risasi Mwaulanga wameliambia gazeti hili kwamba kesho watahutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, waliouandaa ambao pamoja na masuala mengine, wamesema wataufafanulia umma madhara ya tamko la wanaharakati hao dhidi ya bunge.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, mabalozi wa Amani Forum ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk Walid Kabourou, Mrema na Mwaulanga walisema tamko hilo la wanaharakati ni miongoni mwa viashiria ambavyo vimeanza kuonekana yakiwemo maneno ya chini chini ya kuvunja amani ya nchi.

  Katibu wa Amani Forum, Mwaulanga alisema katika mkutano wa hadhara wa kesho ambao ni wa kwanza kufanyika tangu umoja huo uzinduliwe rasmi mwezi uliopita, mabalozi hao wamesema watahakikisha wanaueleza umma pia athari za maneno ya chini chini ambayo yamekuwa yakijitokeza kuhusu masuala ya dini.

  Mwaulanga alisema wanaharakati na vyama vya siasa, vimekuwa vikitoa mfano wa Marekani katika harakati zao lakini vikishindwa kubaini kwamba wao hufanya mambo kwa maslahi ya nchi na maendeleo.

  Alisema katika kuhakikisha kuwa umma unaelewa ukweli wa mambo juu ya suala zima la kulinda amani, Amani Forum mwezi ujao itafanya mikutano mingine miwili Dar es Salaam katika maeneo ya Manzese na Buguruni kabla ya kuhamia kwenye mikoa aliyoitaja kwamba ni yenye utata.

  Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mara, Arusha, Mwanza, Mbeya na ya Kusini. "Uamuzi wa wanaharakati hauna chochote zaidi ya kujenga hisia za chuki na wananchi kutoiamini serikali na bunge lao," alisema Mwaulanga na kusisitiza kwamba badala ya kuandamana, wangekwenda kujipanga wachaguliwe wabunge wanaoendana na matakwa wanayohitaji na si kuandaa maandamano nchi nzima.

  Mwaulanga ambaye maoni yake yaliungwa mkono na Mwenyekiti wa TLP, Mrema, alisema kupitia wanaharakati, wanaweza kujipitisha watu wengine wenye malengo maalumu ya kiuchumi au kisiasa wakapitisha maazimio kwa wananchi yanayoweza kuiingiza nchi kwenye mgogoro.

  Katibu huyo wa mabalozi wa amani ambaye alisema mkutano wa kesho utazungumzia pia mauaji mkoani Mara, alisema wanaharakati walipaswa waandamane kupinga ukatili kama uliojitokeza hivi karibuni wa watu 17 wa ukoo mmoja kuuawa katika Kijiji cha Buhare, Mara na si kujielekeza kwenye mambo ya kisiasa.

  "Umeona hizi taasisi zisizo za kiserikali, zimetangaza maandamano yasiyoisha nchi nzima. Sasa yale maandamano ingawa yanaweza kudaiwa ni dhidi ya bunge, si wangeyafanyia Dodoma bunge linapokuwa pale.

  Lakini unaposema ni maandamano nchi nzima, ni dalili kwamba yanapinga serikali nzima," alisema Mrema. Mrema alisema, "ukishasema maandamano ni nchi nzima, ni dhahiri polisi itakataa. Wakishakataa si dalili ya mgogoro umeanza.

  Yale maandamano yakikosa udhibiti, badala ya kuwa dhidi ya Bunge, wapo watu wanaweza wakajipitisha kumbe wamemlenga Kikwete. Si itakuwa kama Madagascar?." Kiongozi huyo wa upinzani alitetea uamuzi wa Bunge kufunga mjadala wa Richmond na kusema serikali imeshaonesha uwajibikaji kwa kitendo cha Rais Kikwete kuridhia mawaziri wake kujiuzulu.

  Hizi choko choko ni za nini?," alihoji Mrema na kukumbushia kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere huku akisisitiza kwamba watu wanaohamasisha chuki lazima umoja wao ukemee vinginevyo nchi itasambaratika.

  Mrema alisema maeneo mengine ambayo mikutano yao itayazungumzia, ni juu ya maneno ya chini chini kuhusu masuala ya dini ambayo yanaashiria kuleta mgawanyiko. Alisema suala la Mahakama ya Kadhi na mchakato wa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ni miongoni mwa mambo ambayo watayatolea ufafanuzi zaidi ili kuondoa hali ya kukinzana miongoni mwa wakristo, waislamu na Serikali.

  "Wapo wakristo wachache ambao wamekuwa wakinung'unika kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC wakidai kwamba serikali inataka kuisilimu nchi na wakati huo huo wapo waislamu wachache ambao wamekuwa wakidai kwamba nchi inaongozwa na wakristo.

  Sasa haya ndiyo mambo ambayo tumeona tukate mzizi wa fitna kwa kuuweka bayana umma uachane na mawazo haya ya udini, kwani sisi sote ni kitu kimoja. Isije tukaingia kwenye maafa makubwa," alisema Mrema. Mrema alionya kile alichosema ni kumletea chokochoko Rais Kikwete.

  Alisema kitendo cha kumwondoa Rais kabla ya muda wake ambao Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijiwekea, kinaweza kikaleta vita. "Rais hachezewi. Kikwete mkimtishia nyau mnadhani hawezi kukitosa CCM? Katiba inampa madaraka makubwa, akitangaza

  Mwaulanga akizungumzia uamuzi wa Mrema pamoja na mwanachama wa NCCR-Mageuzi, Gilbert Ngua kuwa miongoni mwa wajumbe wa Amani Forum, alisema wametimiza majukumu yao ya kusimamia maendeleo tofauti na mtazamo potofu uliopo wa kudhani kwamba upinzani ni kupinga serikali na kuunga mkono walio tofauti na serikali na chama tawala na kuwaona wanaounga mawazo ya seriakali kwamba wanatumiwa.

  Mwanachama mwingine katika umoja huo wenye idadi ya watu watano, ni Mariam Tawfik. Wiki iliyopita, wanaharakati usawa wa jinsia, haki za binadamu na demokrasia kutoka Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo ya Ukombozi wa wanawake Kimapinduzi (FemAct), walisema Bunge limeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Serikali kutokana na kuridhia kuzika suala la Richmond na Kiwira katika mkutano wake wa 18 uliomalizika. Walitangaza kufanya maandamano nchi nzima.


   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  timu ya kikwete ya kampeni karibu inakamilika sasa................. amebadili mbnu za kusaka ushindi, sasa anawatumia hata wasio wanaCCm anadhihirishaa kuwa "kina mrema wapokwa kazzi maalum"....................

  Mungu ibariki TZ............
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...