Chinese scholarship 2016-2015 information

Wakikuzigua sana design mwenyewe...nilifanya ivyo zamani mambo yalivyokuwa magumu kuipata.
 
Safi sana...nakuunga mkono 100%
 
Sasa mkuu ukisha download hiyo form uliyoijaza csc ina maana unatakiwa uitume hiyo kwenda kwa agency wako ambaye ni hiyo university kwa hiyo hapo inakuwaje?
Mkuu...ukishamaliza kujaza na kuwa na mambo yote yanayoitajika ni kuzituma tu, kwenda chuo (agency husika) kupitia DHL . Ila kama una rafiki yoyote huku unaweza ukamtumia kwy email then yeye akaziprint na kutuma chuo maana kukwepa gharama za DHL.
 
Kuna jamaa mmoja amenimbia kuwa yeye alikusanya vitu vyoote vilivyoitajika ( akajaza online form CSC ila agency number akaandika ya ubalozi wa china) chini kule akaandika vyuo 3 angependa kusoma, then akapeleka pale ubalozini, na amepata udhamini.
 
kwa uzoefu wako mkuu. ipi ni safe? hii ya kupeleka moja kwa moja ubalozi wa china akiwa kama agency au ya ku apply directly kwa chuo husika kikiwa kama agency? Maana mi nataka nipeleke sehemu kwenye probability kubwa ya kupata
 
Una uwezo wa kujaza na kudownload CSC zaidi ya mara moja, lakini hii ya 2 ubadilishe agency number either ubalozi au hicho chuo kingine. Fanya yote kama yapo ndani ya uwezo wako.
 
yeah ni kweli chuo kama Xiamen na vingenevyo vinataka hivyo ila hiyo ni rahisi. nenda chuo ulichomalizia wakuandike barua inayoonesha kuwa major yako ilifundishwa kwa kingereza. ili kupunguza urasimu nashauri draft barua kisha nenda nayo, mana vyuo vyetu kwa urasimu hawajambo wanaweza kukuzungusha kwa uvivu wa kudraft barua. kwa hiyo draft barua kisha ukifika kama hawana sample basi wape hiyo waiweke kwenye headed paper na kisha igongwe muhuri pamoja na sign. mf "....this is to certify that Mr.XXXXX YYY was enrolled in our college from September 1989 to September1992 in a bachelor degree program in computer science taught in ENGLISH.............."
 
kwa uzoefu wako mkuu. ipi ni safe? hii ya kupeleka moja kwa moja ubalozi wa china akiwa kama agency au ya ku apply directly kwa chuo husika kikiwa kama agency? Maana mi nataka nipeleke sehemu kwenye probability kubwa ya kupata
mkuu, dont put all your eggs in one basket. nashauri tuma kwenye vyuo moja kwa moja, apply za wizarani na pia kama kuna nyinginezo omba. usitume sehemu moja tu ukaridhika. pia nikwambie kitu kimoja, pale ubalozini huwa hawatabiriki, there are some friends known to me walipeleka pale ubalozini kisha after some few days wakapigiwa simu na ubalozi waende wakachukue documents zao wazipeleke wizara mana kwa tanzania nominating agent waliopewa "rungu" na ubalozi ni wizara ya elimu. however kuna mwaka kuna mtu alipeleka ubalozin na akapata. wachina hawatabiriki. apply as more as you can to increase your chance
 
Asante kwa ushauri mkuu.. ila kuliko kupeleka wizarani ni bora kuapply moja kwa moja kwa chuo husika. Wizara ya Elimu ya Tanzania siiamini hata kidogo. Ntajaribu kupeleka embassy then wakizingua ntaapply moja kwa moja kwa chuo husika
 
Asante mkuu itabidi nifanye hivo halafu kama uliota vile. Hiko Xiamen ndo nakitaka naona kama kipo powa sana maana kuna course moja matata ya Financial Engineering naona kama imesimamia kucha😛😛
 
HONGERA SANA UBARIKIWE
 
kwa kuwaongezea na vyuo vya Hong Kong karibu vyote vina scholarship kwa ajili ya Mphil na PhD ukituma maombi wakiona unaqualify wanakupa admission na scholarship. andika Hong Kong universities ingia web zao then prosperous students angalia program na mahitaji yao omba tu. wanakupa admission na scholarship. wanatafuta tu wenye qualify basi. Kazi kwenu. Ila vingi deadline huwa ni 1 December na kuna clearance round jaribu bahati yako.
 
Asante sana mkuu kwa taarifa.
 
Tunashukuru kwa taarifa. Zinazopitia Wizara ya Elimu na Wizara ya Nishati pia deadline bado. Wanaoomba oil and gas kupitia Wizara ya Nishati Deadline 17.03.2016
 
Habari wakuu,
Naona vyuo vyote vya china wanataka application fees ili uweze kupata admission. Je, kuna namna yoyote ambayo unaweza kuikwepa hii application fee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…