China yatoa msaada vifaa vya maktaba

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
KAIMU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Selestine Gesimba, ameushukuru Ubalozi wa China nchini kwa kutoa msaada wa vifaa vya maktaba ambavyo vitawasaidia wananchi kuongeza maarifa zaidi.

Bw. Gesimba alitoa pongezi hizo Dar es Salaam jana wakati akizindua chumba cha maktaba ya China kwenye majengo ya Maktaba ya Taifa.

Ubalozi huo ulikabidhi msaada wa kompyuta 19, vitabu, CD, meza, viti na kabaiti za kuhifadhia vitabu ambavyo vina mada mbalimbali zenye masomo yanafundishwa nchini kama Jiografia,” alisema.

Aliongeza kuwa, misaada kama hiyo itolewe na mikoani ili lengo la kutoa elimu kwa wananchi liweze kufikiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Maktaba ya Taifa Bw. Ali Mcharazo, aliwataka Watanzania kwenda kutumia vifaa hivyo.

Balozi wa China Bw. Lu Youqing, alisema chumba hicho kitakuwa cha taaluma, maalifa sambamba na vitabu zaidi ya milioni moja ambavyo vitasaidia kuleta maendeleo.


Alisema kupitia maktaba hiyo Watanzania wataweza kujifunza historia ya China, utamaduni wao na asili ya nchi hiyo.
 
Back
Top Bottom