Huyo alotoa ripoti aliipataje bila kupeleleza?Serikali ya China imekanusha kuwa ripoti iliyotelewa na gazeti binafsi la Ufaransa la Le Monde kuwa imekuwa ikifanya upelelezi dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) yaliopo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Taarifa hiyo ilidai kuwa kwa muda wa miaka 5, habari kutoka jengo la AU, lililojengwa na Wachina, zilikuwa zikipelekwa jijini Shanghai usiku wa manane.
Balozi wa China katika Umoja wa Afrika, Kuang Weili, alitaja ripoti hio kuwa "isiyo na mantiki" na "ya kupotosha."
Pia alitia shaka kwenye siku ripoti hio ilitolewa, ambapo ilitolewa siku moja kabla ya viongozi wa Afrika kuanza mkutano wao wa mwaka katika makao makuu ya Umoja wa Afrika.
Jengo hilo lenye gorofa 20 liligharimu dola za Marekani milioni 200 na limekuwa makazi ya bodi hiyo ya Bara la Afrika tangu mwaka 2012.
Chanzo: BBC Swahili
Mazuzu kabisa sisi. Ila viongozi wetu ndio mazuzu kuliko sisiYaani Mtu akujengee na akukabidhi tu hivihivi, thubutu.
Ila Waafrica kazi tunayo, sasa hapo kinachoendelea ni malumbano kati ya France na China, sie tupo Mtu kati, tunageuka kwa France akiongea, tunageuka kwa China akiongea, sidhani hata kama tuna cha kuchangia.
Yaani Mtu akujengee na akukabidhi tu hivihivi, thubutu.
Ila Waafrica kazi tunayo, sasa hapo kinachoendelea ni malumbano kati ya France na China, sie tupo Mtu kati, tunageuka kwa France akiongea, tunageuka kwa China akiongea, sidhani hata kama tuna cha kuchangia.
Sisi ni mazuzu kuliko viongozi wetu. Sababu mtu asiye zuzu kamwe hatokubali kutawaliwa achilia mbali kuongozwa na zuzu.Mazuzu kabisa sisi. Ila viongozi wetu ndio mazuzu kuliko sisi
Sanaaaa tena umaskini hadi wa akiliUmasikini mbaya sana.
We jamaa unamuono mkubwa sanaSisi ni mazuzu kuliko viongozi wetu. Sababu mtu asiye zuzu kamwe hatokubali kutawaliwa achilia mbali kuongozwa na zuzu.
Waafrika wengi ni first class zuzus
Si ndio hapo sasa.Shutuma zipi ziliwahi kubaliwa?