China yajibu mapigo-Yapandisha kodi kwa bidhaa za USA

Wewe umesoma uchumi gani?, mnunuzi akikataa kununua bidhaa zako unayeumia ni wewe muuzaji soma 'US - china tariff war'
Kumbuka bidhaa karibia zote zinazotoka china kwenda marekani ni za wamarekani wenyewe na sidhani kama wataweza kuzipiga marufuku maana wakifanya hivyo itakua ni kuziua company zao wenyewe

Hapa tunazungumzia company kuanzia hp,dell,apple,textiles

Company kubwa zote za USA zinazalishia bidhaa zao china na bidhaa zikitoka china na kwenda usa zinahesabika kama imported goods ilhali ni bidhaa zao wenyewe wamarekani na zinawaletea faida vile vile wakina apple na wengineo na kadiri ushuru unavyozidi consumers wamarekani nao wanapata mzigo mkubwa vile na china nao watapunguza export

Hapa mkuu hakuna atakaye win kwenye hii battle,hapa nilimjibu jamaa kwa nini china amerespond tarrifs ndogo kwa USA ni kwa sababu tu hawa wana balance of trade isiyo sawa yani kuna mmoja anapeleka bidhaa nyingi kwa mwenzake kuliko mwingine
 
Wewe umesoma uchumi gani?, mnunuzi akikataa kununua bidhaa zako unayeumia ni wewe muuzaji soma 'US - china tariff war'
Marekani hawezi kukataa kununua bidhaa zake mwenyewe

Kwa akili yako marekani na wamarekani wanaweza kukataa kununua apple products au hp computers au hata nguo za michezo zile nike?
 
Itakua uchumi alifundishwa na mwalimu wa kemia
 
Sema kitachomkwamisha ni kwamba viwanda vingi vikubwa vya marekani vipo china labda akitaka awe sawa hivyo viwanda ni kuvirudisha nyumbani ila kuzidi kuongeza tarrifs ni kuwaumiza tu consumers wa marekani na vile vile nilisikia kwamba marekani inataka kuhamimishia viwanda vyake india na ikifanya hivyo yatakua ni yale yale tu yani karuka mkoja na kakita nyesi maana na india nayo itaendelea na ita acquire technology na USA tena itaanza kuona wivu kama ilivyo kwa china

Hapa solution ni kuhamishia viwanda vyote virudi kwao na hapo ndio waanze kushindana kufanya biashara na kwa jinsi usa ilivyo soko la ushindani kwao litakua gumu sana bidhaa zao ni ghali sana kama watazalisha wenyewe.
 
Kudump treasury ni last resort kabisa na sidhani kama china watafanya hivyo kwa sasa na ikitokea wamefanya italeta impact kubwa sana kwa pande zote na usa ki ukweli haita kopesheka kabisa na nchi nyingi zita dump us treasury.
 
Chief unamwaga nondo ambazo mtu asieujua uchumi anaweza kutokukuelewa...

Wote wataloose kwenye hii vita yao ya kiuchumi ila tatizo wengi wetu tumejaa ushabiki zaidi kuliko uhalisia
 
China ndio nchi yenye purchasing power parity (PPP) kubwa kuliko nchi yeyote ile duniani.
Nimegoogle nikaona nikataka niyaondoe niliyoandika lakini umakonda ukaniingia na sikubali china haiwezi bila export!
 
Maana yake hapo atakaye athirika zaidi ni mchina maana anamtegemea zaidi mmarekanikuliko mmarekanian avomtegemea mchina

Wanaoumia zaidi ni wananchi wa marekani, kwa kuwa watapata bidhaa zile zile ambazo zinatengeneza china kwa gharama kubwa, production cost ya bidhaa per unit kwa marekani na china ni tofauti sana, china more cheap na matajiri wa US wamegoma kurudisha viwanda ndani kwa sababu ya gharama kubwa za uzalishaji, Marekani anaongeza tariff kwenye hadi malighafi za uzalishaji wkati mwenyewe hana uwezo wa kupata hizo malighafi kwa viwanda vya ndani...marekani hawezi kuepuka bidhaa za china
 

Kumbuka pia wawekezaji wakubwa China Ni wamarekani ambao wanapeleka nyumbani ile faida wapatayo huko China.

Lakini pia Marekani hawezi kupata mbadala wa bidhaa zake zitokazo China. Mfani Apple, Hp, etc products Ni za kimarekani zinazozalishwa China, kusema zitakosa soko sehemu ingine duniani Ni uongo lakini mbadala wake kwa wamarekani pia haupo.

Hapa ndipo utaona Kila mmoja anamuhitaji mwenzake na maumivu kwa mmoja Ni maumivu kwa wote.

Hivyo Ni zero sum game
 
Hapa china kwa vyovyote vile lazima asalim amri hamna jinsi
 
Kudump treasury ni last resort kabisa na sidhani kama china watafanya hivyo kwa sasa na ikitokea wamefanya italeta impact kubwa sana kwa pande zote na usa ki ukweli haita kopesheka kabisa na nchi nyingi zita dump us treasury.
Marekani hakopi,ila nchi zinanunua Deni lake. Hata Urusi inamiliki sehemu ya Deni la Marekani. Wanaoongoza ni China na Japan
 
Mbadala wa mnunuzi ni mkubwa ukilinganisha na wa muuzaji.
Hizo bidhaa zinazozalishwa China wawekezaji wakiona hawapati faida wanaweza kuamua kuhamisha viwanda vyao kwenye nchi nyingine za karibu Kama vile India, Indonesia,Taiwan,nk zikaenda Marekani.
Je kwa China?!
 
Kukiwa na vita ya kibiashara kati ya nchi mbili, kwa kutunishiana misuri kama ifanyavyo USA na China, basi asilimia kubwa yule ambaye amekuwa akiuza zaidi kwa mwenzake ndiye ataathirika zaidi.

Wabobezi wanasema USA ni mwagizaji mkuu wa bidhaa toka China. Pia hawahawa wataalamu wanasema pamoja na US kukaza msuri kwa China na kisha China kulipiza, bado dollar ya Kimarekani inazidi kupata nguvu. China hawezi kaza sana msuri kwa sababu yeye si mnunuzi mkubwa toka USA.

Wataalamu wanasema ingawa China inaweza kuathiri mauzo ya kampuni za USA zilizopo ndani ya China kama Apple na GM, bado iPhone zinazouzwa China zinazidi zile zinazouzwa USA na kampuni ya magari GM inauza magari zaidi nchini China kuliko USA.

Wataalamu waliomo humu labda watatujuvya zaidi.

 
Unajua china inapeleka bidhaa za thamani kiasi gani USA na USA inapeleka kiasi gani china?

Unataka china nao waweke hizo tarrifs za billion 200 na wakati hawajafika huko kwenye uthamani wa hizo bidhaa
Soko kubwa la mchina ni USA, So mchina anamhitaji zaid mmarekani kuliko mmrakani anavyomhitaji mchina.

Nope:
wote wataumia lakni mchina ataumia zaidi kuliko atakavyoumia USA.
 
Hii comment yko imenifikirisha zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…