Tengero
Member
- Feb 9, 2017
- 75
- 54
Katika kuimarisha Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nchi yetu ya Tanzania na Nchi ya China, Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (SUKI) Comred Ngemela Lubinga siku ya jana tarehe 16.01.2018 alikabidhi zawadi kwa Balozi wa China nchini Tanzania Bi Wang Ke.
Comred Lubinga alikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Uongozi wa Shule ya Msingi Bweyunge iliyopo wilayani Misenyi na wanafunzi wa shule hio waliotoa zawadi kama sehemu ya shukrani kwa balozi wa China kwa msaada wa fedha wa zaidi ya shilingi millioni 23.
Pamoja na zawadi kutoka Shule ya Msingi Bweyunge Comred Lubinga alikabidhi ramani za michoro ya jengo la CCM mkoa wa kagera na jengo la CCM wilaya ya Misenyi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo za chama.
Katika Mazungumzo na Balozi huyo Comred Lubinga alimkaribisha Bi. Wang Ke kuja kuwekeza katika Mkoa wa Kagera hasa katika sekta za kilimo kwani kuna fursa ya uwepo wa mazao ya biashara kama vile kahawa na mazao ya chakula mfano Ndizi,Mpunga na mahindi.
Comred LUbinga pia alimweleza balozi Wang Ke kuwa katika wilaya za Karagwe na Misenyi kuna fursa ya uwekezaji katika sekta ya madini ambayo kwa sasa wapo wachimbaji wadogo wadogo ambao wanachimba kwa kutumia teknolojia duni hivyo ni muhimu kupeleka teknolojia ya kisasa katika uchimbaji wa madini hayo.
Naye balozi wa China alionyesha nia ya kutaka kuwekeza katika sekta ya madini Mkoani Kagera na ameahidi kutembelea Mkoa huo ili kujionea fursa zilizopo katika Mkoa huo na namna bora ya kuwekeza.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuimarisha mahusiano yake ya kisiasa na kiuchumi na Nchi mbalimbali ikiwemo Nchi ya China ili kuweza kujenga maendeleo baina ya Nchi hizo ambayo yatapelekea maendeleo ya mtu mmoja na mmoja na hatimaye Taifa kwa ujumla.