China na Urusi zaungana kuikabili Marekani

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,952

Uongozi wa Jeshi la China umeahidi kuisaidia na kuiunga mkono Urusi kijeshi kukabiliana na mataifa ya Magharibi dhidi ya mzozo wa kidiplomasia, vikwazo vya kiuchumi na mazoezi ya kijeshi.

Ahadi hiyo imetolewa Waziri wa Ulinzi wa China, Wei Feng ambaye yuko Urusi kuhudhuria mkutano wa saba wa kimataifa wa usalama wa Moscow akiwa ameambata na ujumbe wa maofisa wa ngazi za juu wa jeshi.

Feng alisisitiza kwamba ziara yake imeratibiwa moja kwa moja na Rais wa China, Xi Jinping.

Alisema alikwenda Moscow akiwa na ujumbe maalumu kutoka kwa Jinping katika kipindi hiki ambacho mataifa yote mawili yanaboresha majeshi yao na ushawishi wao duniani licha ya wasiwasi wa Marekani.

“Naitembelea Urusi kama waziri mpya wa ulinzi wa China kuionyesha dunia maendeleo ya hali ya juu ya uhusiano wetu na dhamira imara ya majeshi yetu kuimarisha ushirikiano wa kimkakati,” alisema Wei wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergey Shoigu.

“Pili, kuisaidia Urusi kuendesha mkutano wa kimataifa wa usalama wa Moscow ili kuwaonyesha Wamarekani uhusiano wa karibu wa majeshi ya China na Urusi hasa katika hali ya sasa.

“Tumekuja kuwaunga mkono katika harakati zenu na hali inayowakabili,” aliongeza.

“Upande wa China uko tayari kuzungumza na Urusi kuhusu wasiwasi na misimamo yetu ambavyo vinawiana dhidi ya matatizo ya kimataifa katika majukwaa ya kimataifa pia,” alisema.

Hali hiyo inakuja huku mataifa hayo mawili yakiingia katika mzozo na Marekani katika maeneo tofauti kuanzia kijeshi hadi kiuchumi.

Rais Vladimir Putin wa Urusi na Jinping wa China wanaongoza kile kinachohesabiwa kuwa majeshi yenye nguvu yanayoshika namba mbili na tatu duniani nyuma ya Marekani.

Wakati Marekani imeendelea kuongoza kwa kipindi kirefu ikiwaacha kwa mbali washindani wake linapokuja suala la kijeshi, Moscow na Beijing zinakuja juu haraka zikilenga kuondoa pengo hilo na kudhibiti ushawishi wa Marekani katika siasa za dunia.
 
washirika wa Urusi.
1.China
2.Cuba
3.Iran
4.North Korea
5.Venezuela
6.Syria
7.Bolivia
Washirika wa Marekani.
1.UK
2.Germany
3.France
4.Japan
5.South Korea
6.Israel
7.Canada
Piga hesabu mwenyewe ni nani atashinda vita?
 
ukiangalia vizur progress ya china kiuchumi na kijeshi toka 1980's hadi 2018 ni kubwa sana!! Sio kwamba kamzidi US bali ni tishio sana kwa US na ukizingatia nchi za ulaya zimegundua mshikamano wao na US unamnufaisha Us kuliko wao!!
China na Russia North Korea ni tishio kubwa kwa NATO.
 
hivi germany ni mshirika wa US ? Of course najua US has millitary base in germany
 
washirika wa Urusi.
1.China
2.Cuba
3.Iran
4.North Korea
5.Venezuela
6.Syria
7.Bolivia
Washirika wa Marekani.
1.UK
2.Germany
3.France
4.Japan
5.South Korea
6.Israel
7.Canada
Piga hesabu mwenyewe ni nani atashinda vita?
tanzania tuko upande wa nani?
 
washirika wa Urusi.
1.China
2.Cuba
3.Iran
4.North Korea
5.Venezuela
6.Syria
7.Bolivia
Washirika wa Marekani.
1.UK
2.Germany
3.France
4.Japan
5.South Korea
6.Israel
7.Canada
Piga hesabu mwenyewe ni nani atashinda vita?

Hapo Japan, Germany na DRK hao sio wakuwategemea maana hao wote wanauchungu wakihistoria na marekan, wamekaa kimya na kujifanya wanamsikiliza ili tuuu mambo yao yaende sawa, ila awawezi kubali kuumia kumkomboa marekan
 
washirika wa Urusi.
1.China
2.Cuba
3.Iran
4.North Korea
5.Venezuela
6.Syria
7.Bolivia
Washirika wa Marekani.
1.UK
2.Germany
3.France
4.Japan
5.South Korea
6.Israel
7.Canada
Piga hesabu mwenyewe ni nani atashinda vita?
Mjermani ana mahusiano na urrusi ktk masuara ya kijasusi,kuna kipindi mjerumani aliwahi kupewa taarifa na K.g.b. ya urussi kuwa awe makini anapelelezwa na marekani kuna kipindi ufaransa na ujerumani ziliwahi kuishutumu sn marekani na zilitoa matamko makali sn.
 
Vita ya maneno tu.... wapigane tujue kiongozi wa dunia nani isiwe kurushiana maneno tu kama khadija kopa
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
halafu Simba akigeuka akaunguruma tu wote nduki
[emoji23] [emoji23] [emoji23] halafu Simba akigeuka akaunguruma tu wote nduki
Kwa komenti kama hizi ndo zinawafanya watu wakuone kuwa ni mshabiki wa Marekani badala ya kukuona kama mseama ukweli.Kuna tofauti kati ya shabiki na msema kweli.Kwa komenti hii hata Wamarekani orijino watakukana.
 
washirika wa Urusi.
1.China
2.Cuba
3.Iran
4.North Korea
5.Venezuela
6.Syria
7.Bolivia
Washirika wa Marekani.
1.UK
2.Germany
3.France
4.Japan
5.South Korea
6.Israel
7.Canada
Piga hesabu mwenyewe ni nani atashinda vita?
Umesahau kuwa India ni rival wa China, so in any case ata side na Marekani...
 
Back
Top Bottom