China na Urusi zashtumiwa kuendelea kuiuzai mafuta Korea Kaskazini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Maafisa wawili wa usalama barani Ulaya wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba malori mawili ya mafuta kutoka Urusi yaliwasilisha mafuta huko Korea Kazkazini hivyo kukiuka azimio la umoja wa mataifa la kuzidisha vikwazo zaidi dhidi ya utawala huo wa Pyongyang ili kujaribu kukomesha mradi wake wa kutengeneza silaha za kinuklia.
_99404998_774f7caa-d730-4e42-aa57-e5654e5743f6.jpg

Wanasema malori hayo yaliyosafirishwa kwa meli yalionekana katika picha za Satellite zilizo karibu na bandari za Urusi upande wa pwani ya Pacific na kuthibitishwa kwa duru za kiintellijensia .

Hata hivyo mmoja wa maafisa hao ameongeza kusema kuwa bado hamna ushahidi wowote kwamba serkali ya Urusi imehusika na usafirishwaji wa shehena hiyo.

Meli husika ambayo iko chini ya leseni ya Hong Kong ilikamatwa na maafisa wa Korea Kusini lakini mwenye meli hiyo amekana kuhusika na swala hilo.


Rais Trump aishutumu China kwa kukiuka vikwazo vya UN dhidi ya Korea Kaskazini
_99400921_trumptweeeet.png.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amevunjwa moyo na China kufuatia ripoti kwamba iliruhusu mafuta kusafirishwa hadi nchini Korea Kaskazini.

Katika Ujumbe wa twitter, bwana Trump alisema kuwa China ilionekana ''hadharani'' ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini.

Amesema hakuwezi kuwa na suluhu ya kirafiki katika mgogoro wa Korea Kaskazini iwapo mafuta yataruhusiwa kusafirishwa hadi Pyongyang.

China mapema ilikana kwamba kumekuwa na ukiukaji wowote wa azimio la Umoja wa mataifa la mafuta kati ya China na Korea Kaskazini.

Wiki iliopita , Beijing iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90.
Vikwazo hivyo vikali ni jaribio jipya kuzuia majaribio ya silaha yanyotekelezwa na Pyongyang.

Matamshi hayo ya rais Trump dhidi ya China yanajiri baada ya gazeti moja la Korea Kusini Chosun IIbo kuripoti kwamba meli za China zimekuwa zikisafirisha mafuta kwa siri kupitia baharini kuelekea Korea Kaskazini.

Likiwanukuu maafisa wa serikali ya Korea Kusini, limesema kuwa usafirishaji huo unaenda kinyume na sheria kutoka meli moja hadi nyingine ulipigwa picha na Satellite za Marekani za ujasusi takriban mara 30 tangu mwezi Oktoba.

Maafisa wa Marekani hawakuthibitisha ripoti hiyo lakini afisa ya idara moja ya serikali aliyenukuliwa na reuters alisema kuwa usafirishaji huo huenda unaendelea.

Usafrishaji wa mafuta kutoka meli moja hadi nyingine unaendelea kuleta wasiwasi ikiwa miongoni mwa njia za Korea Kaskazini kukwepa vikwazo hivyo.

China ambayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa taifa la Korea Kaskazini , imesema kuwa inatekeleza vikwazo vyote vilivyowekwa na UN dhidi ya Korea Kaskazini.
_99400923_65ac026c-4a37-4e07-bd63-68c05f70fde9.jpg

Haki miliki ya picha AFP


Chanzo: BBC Swahili
 
China na Urusi kamwe hawatozuia kupeleka mafuta NK ,..vikwazo vyote hutekeleza lkn kuhusu mafuta hawatoacha kamwe kuwapelekea NK

Hili lipo wazi
 
Trump namshauri akate misaada kwa China na Urusi... kama alivyo fanya kwa nchi zilizo ipinga ktk suala la Jerusalem
 
U.S. aache kulalamika aingie vitani amalize tatizo kama anaweza mbona Iraq aliingia!!
mziki wa kim lazima ajishauri mara mbilimbili laa sivyo washington inageuka majivu sasa hivi.makombora anayorusha kiduku siyo ya duniani.
 
Trump namshauri akate misaada kwa China na Urusi... kama alivyo fanya kwa nchi zilizo ipinga ktk suala la Jerusalem
Dogo usidhani mnavyopokea misaada huku afrika na kwengine ni hivyo hivyo. 75 % ya bidhaa zinazoingia US zinatoka China
 
Dogo usidhani mnavyopokea misaada huku afrika na kwengine ni hivyo hivyo. 75 % ya bidhaa zinazoingia US zinatoka China
Mkuu ilikuwa ni namna ya kumpa kichwa kichaa ili afanye yale anayo amini kwake ni sahihi... hakuna hasiyejua nguvu aliyo nayo china, urussi, japani, germany ktk uchumi
 
siyo hawezi ni kwamba hana uwezo huo. China ni taifa la pili kwa nguvu ya kiuchumi duniani ataisaidia nini China? wanategemeana
Hahahahha exactly mkuu U.S. hana ujanja kwa sasa!!!
china katengeneza ndege lake halijulikani ni la kuokoa tu au lina malengo mengine mengine !!
 
Hivi humu ndani kuna vichaa? Kubwa zima unasema US asipeleke misaada CHINA na URUSI? Hivi una habar kama China inamdai US billions of $ na bado anaruhusiwa kukopa kama akihitaji? Low Level mind dude! Kama anaubavu akaiteke meli ya urusi itakayopeleka mafuta au aiteke meli ya Korea kaskazini kama hatokula kerbu
 
Back
Top Bottom