China kukataa Uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa, ni kupambana na ubabe wa Nchi za Magharibi?

CRI Swahili

Member
Dec 21, 2013
19
42
Mahakama maalum ya utatuzi wa migogoro(PCA) hivi karibuni ilitoa uamuzi wa kesi kati ya China na Philippines, iliyowasilishwa na Philippines kwenye mahakama hiyo kutaka ufafanuzi kuhusu uhalali wa eneo la mpaka wake na China kwenye eneo la bahari ya China kusini.

China imepinga uamuzi uliotolewa wiki hii na mahakama hiyo, unaokosoa mpaka wa China kwa madai kuwa Philippines ilifungua kesi kinyemela bila kuwasiliana na China kama utaratibu wa sheria unavyoagiza, mbali na kuwa uamuzi wenyewe unaenda kinyume na ukweli.

Mwaka 2013 China ilitangaza kukataa kushiriki kwenye kesi hiyo, kwa madai kuwa mahakama hiyo imevuka mamlaka iliyopewa kisheria. Lakini mwaka jana PCA ilisema ina mamlaka.

Kati ya majaji watano wa mahakama hiyo, wanne wanatoka nchi za Ulaya, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi na Poland, na mwingine anatoka Ghana ambaye anaishi Ulaya. Hakuna hata mmoja anayetoka Asia ambako ndio kuna mgogoro.

Nini maoni yako? (Tutayasoma maoni yako katika vipindi vyetu kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa)
 
Back
Top Bottom