Chiligati na Mrema wanamhujumu Lissu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chiligati na Mrema wanamhujumu Lissu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Apr 4, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kesi ya kupinga matokeo ya Lissu yaibua mambo mazito.
  Chiligati atajwa kuhusika kuandaa ushahidi,
  Mrema na mwanae watumika kusaidia CCM kumpinga Lissu,
  Mashahidi waingia tena mitini, jaji aamuru walipe gharama.
  Josephat isango- Singida.
  Kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA jana iliibua mambo mapya, baada ya mshitakiwa Tundu Lissu kutoa waraka Mahakamani ulioandikwa na John Chiligati kuomba ufafanuzi namna TLP ilivyoshiriki katika uchaguzi Mkuu wa 2010.
  Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo Tanzania daima inayo, yenye kumbukumbu namba CCM/OND/559 Vol.II/10, ya tarehe 23/03/2011. John Chiligati aliomba kujua kama kweli TLP iliweka mawakala katika Jimbo la uchaguzi wa singida mashariki, au kama mihuri iliyotumika ya TLP ilikuwa ni sahihi au ni ya kughushi,

  Kufuatia barua hiyo, barua nyingine ya majibu kwa Chiligati, iliyotolewa mahakamani hapo na Tundu Lissu ilitoka kwa Hamadi R. Tao, aliyekuwa naibu katibu Mkuu TLP, yenye kumbukumbu Namba TLP/HQ/HAB/VOL.V/165, Ilisema Ni kweli mawakala wa TLP hawakuteuliwa au kama waliteuliwa utaratibu wa uteuzi haukufuata taratibu za Chama. Barua hiyo ya TLP ilipingana vikali sana na barua ya Mwenyekiti wa TLP, wilaya ya singida, iliyoandikwa kumjibu Katibu wa taifa wa TLP, ya tarehe 12/04/2011, ilisema kuwa Chama cha TLP kiliweka mawakala kusimamia katika uchaguzi Mkuu bila malipo.
  Hata hivyo mjadala wa mahakamani ulikuwa Mkubwa, baada ya Shahidi wa 19, Bw. John Madindilo, ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa singida kukubaliana na hoja zote za Lissu, na alimtaja Mtoto wa Augustino Mrema, anayeitwa Michael Mrema kuwa alitumwa singida kama afisa wa Chama kwenda kufuatilia suala hili, na alipopewa taarifa hiyo, hakuridhika nayo badala yake aliwalelekeza wale viongozi wa Singida, kuandika barua kwa Katibu Mkuu kadiri itakavyompendeza Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema.
  Baadhi ya mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: Baina ya tundu Lissu na SHAHIDI, JOHN MADINDILO
  T/L Ni kweli au si kweli kuwa ulikasimu madaraka kwa Mwenyekiti wa TLP wa wilaya ya Singida, kwa kuwa wewe ulikuwa Mgombea, na Mwenyekitji wa Wilaya ya singida, ulimwamini, kwa uwezo wake na uadilifu , na uzoefu wake?
  P/W:NDIYO NILIFANYA HIVYO LAKINI YEYE PIA YUPO MAKAO MAKUU YA MKOA HAPA MJINI.
  T/L Ni kweli au si kweli kuwa mliweka mawakala kulinda maslahi ya Chama,
  P/W NI kweli,
  T/L Ni sahihi au siyo sahihi, mnapokuwa na Mgombea urais, huwa mnaweka mawakala?
  P/W NI KWELI, pale ambapo mawakala wanakuwa tayari kujitolea.
  T/L Ni kweli au si kweli kuwa kwa mujibu wa barua ulizo nazo, kesi hii ipo kwa maslahi ya Chiligati na Mrema?
  P/W Ni kweli kwa mahusiano ya barua hizi walizoandikiana.
  T/L Kama nimekusikia vizuri uliiambia mahakama hii kuwa kuna Afisa wa Chama anakuja toka Mkao makuu, umpokee na umpe ushirikiano?
  P/W NI kweli.
  T/L Je huyo afisa wa chama alikuwa anaitwa nani?
  P/W: Siruhusiwi kumtaja
  JAJI: Kama umemtaja Augustino Mrema, Mwenyekiti wa TLP Taifa ni Afisa gani unashindwa kumtaja
  P/W: ni Mikaeli Mrema.
  T/L. Mikaeli Mrema ambaye ni mtoto wa Augustino Mrema?
  W/P.NDIYO
  T/L. Mikaeli Mrema alisema nini?
  P/w; alisema kuwa kulikuwa na mawakala hewa wa TLP waliwekwa Singida mashariki?
  T/L. Hukushangaa kupokea taarifa ya Malalamiko toka makao makuu wakati wewe Mwenyekiti wa Mkoa huna taarifa yeyote?
  P/W: NILISHANGAA SANA lakini nilipokea kwa kuwa inatoka kwa Mkubwa wangu wa Kazi.
  T/L: Nimeshtakiwa hapa, kwa mujibu wa barua mbalimbali ulizosoma, wanaitaka Mahakam itengue matokeo ya uchaguzi, kwa mujibu wa ufahamu wako, unasemahe juu ya hili?
  P/W: watakuwa wanakuonea.
  Kesi hiyo haikuendelea mchana, baada ya upande wa walalamikaji kushindwa kuleta Mashahidi mahakamani, kitendo kilichopelekea jaji kuwapiga faini ya kulipa nusu gharama ya siku katika kesi hiyo:
  Na mahojiano yalikuwa hivi:
  Wakili wa walalamikaji; Mheshimiwa jaji, naiomba Mahakama iahirishe kesi hii hadi kesho kwa kuwa shahidi wetu hajaja, na amefunga simu,
  JAJI: Ulichukua hatua kuleta shahidi mmoja tu?
  Wakili: huwa tunachelewa kutoka mahakamani, hivyo inakuwa vigumu kuwatafuta kwa siku inayofuata. Hata hivyo kazi ya kutafuta mashahidi sio yangu ni ya wateja wangu.
  TUNDU LISSU: Mheshimiwa jaji, uchelewashaji unaofanywa kwa makusudi unaniathiri mimi, kwanza kiuchumi kwa kuwa nakaa hotelini, pili ninashindwa kushiriki kazi za kibunge, na ninashindwa kuwatumikia wanachi wangu walionichagua. Siku nyingine ulinionya nisidai gharama, leo mheshimiwa jaji, naomba upande wa walalamikaji walipe gharama,
  Jaji: Mlalamikaji naomba usimame, unajua kuwa katika kesi hii mimi nalipwa na serikali, na hawa wanasheria watatu wa serikali, na katibu wangu?
  MLALAMIKAJI: NDIO,
  JAJI: mbona hampo ‘serious’ . Kuna uzembe mkubwa unatokea na leo hii sitaki kukubali kirahisi uzembe huu. Kuna uzembe unafanywa na walalamikaji, na tayari nilionya hili tangu mwanzo. Mtumzembe hukumbushwa na leo naamuru mtalipa nusu gharama ya ahirisho la kesi leo kwa uzembe wenu ili mjitume na mjue wajibu wenu sio kutupotezea muda hapa.
   
 2. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  Hamna kesi hapo! ni kupotezeana muda tu..
   
 3. M

  MADORO Senior Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwanini mpaka sasa, hata NJAU ambaye ndiye alikuwa Mgombea hajaja, hata kuwa shahidi, tumsikilize yeye kuliko kupata maoni ya wanakijiji, wazee wanaosumbuka kwa sababu ya Mawazo ya Chiligati na Mrema?
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  kumbe unaweza kuwa mshitakiwa na ukasimama kama mwanasheria kujitetea?watamweza lissu hao vilaza kweli?
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  vakhojanga avai! Mbwa-amunio he urii!
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Mrema nashindwa kumlaumu sababu huwa namchukulia kama the walking dead, Badala ya kutumia muda wake mwingi kujitibia na kumuomba Mungu neema ya Uzima zaidi na zaidi yeye anafikiria waliompush akaangukia pembeni ya shimo la kaburi ni CCM.

  Nashindwa kuelewa, kama watu ambao wanashikiria nafasi kubwa za uongozi kwenye Taifa letu hawana ufahamu wa misingi thabiti ya maisha ya furaha na amani hawa wananchi masikini kabisa waliopitwa na raha nyingi za ulimwengu huu hali yao iko vipi?

  Hivi kweli kabisa, Mrema anadiriki Kuifanya CCM ndio Mungu wake?? CCM ni Mungu kweli? CCM?
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu hawa wanao peleka kesi mahakamani bila ushahidi sindio kweli hizi pesa za serikali kodi za wananchi zatumika vibaya sasa

   
 8. N

  Ndisila Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I expected Tundu Lissu to be as smart as ever. He is conduction the case on his own and I can see how these so called witnesses for the Petitioners conceeding to the obvious. What more? it is a total waste of Tax Payers money just to please disgruntled losers and their Allies like Chilli sauce opps! gati. Keep it up Tundu.
   
 9. m

  maviazi Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri wakati mwingine mahakama iwe inatoa adhabu kali kwa walalamikaji wasio na mashahidi kama hii ya lissu
   
 10. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huyo jamaa in red ni mwoga, amejificha nyuma ya hao wanakijiji na ukweli ni kwamba anawatumia hao wanakijiji kutimiza malengo yake. Hiyo kesi amewaandalia kila kitu wanakijiji wakafanya kusaini tu.
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Arguing with a lawyer is like mud wrestling with a pig, at the end of the day the pig enjoys it. kwa TUNDU LISSU WAMECHEMKA!
   
 12. Y

  Young zee JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 398
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapa hakuna kesi,
  Toka mwanzo upande wa walalamikaji wanashindwa kutunza muda. Pia hawakujiandaa kiushahidi.Hivyo basi Jaji anatakiwa kuitupilia mbali hili shauri
   
Loading...