Chiligati: Atishia kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chiligati: Atishia kujiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tembeleh2, Feb 29, 2012.

 1. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Source: mwananchi 29/2/2012
  Wana JF hebu angalieni majibu haya ya Mh. Chiligati halafu mchangie. Mimi nafikiri hana ubavu wa kujiuzulu, nyie je?

  Alipoulizwa jana kuhusu tishio lake la kutaka kujiuzulu Chiligati alisema: "Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe." Mahojiano yake na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

  Swali: Salaam ndugu Chiligati. Kwanza heri ya mwaka mpya.
  Jibu: Nzuri, nashukuru na wewe pia.

  Swali: Nimesikia kuwa juzi ulitaka kujiuzulu ujumbe wa sekretarieti kutokana na kuvuja siri za kikao chenu cha juzi cha mchakato wa kura za maoni wa Arumeru Mashariki je, msimamo wako ukoje hadi sasa hivi?
  Jibu: Bwana wewee! Sikia, hayo ni mambo ya ndani ya vikao. Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe!

  Swali: Sawa, natambua ni la vikao vya ndani vya chama, lakini huoni kuvuja kwa siri za vikao vyenu kunaonyesha sekretarieti imegawanyika?
  Jibu: Nakwambia hivi, hayo ni mambo ya ndani ya vikao. Kwani wewe mbona hutuambii mambo ya nyumbani kwako na mkeo?

  Swali: Hujaniuliza, ungeniuliza ningekwambia. Lakini, je, sasa kama siri zitaendelea kuvuja msimamo wako utakuwa ni upi?
  Jibu: Haaah...! Wewe bwana shughulika na ya kwako, haya hayakuhusu. Haya ni sawa na mambo ya ndani ya nyumba, ni yetu wenyewe tutayazungumza kwenye vikao vyetu.

  Swali: Lakini, tayari mmeweza kubaini ni vipi siri za vikao vyenu zinavuja na labda mmejua ni nani anayezivujisha?
  Jibu: Nasema tuachie wenyewe, hatutaki utuingilie. Nasisitiza tena kitu kimoja, hilo halikuhusu endelea na mambo yako.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ha ha haa!
  Huyu yuko kama Chemical Ali!...hakubali uwepo wa tatizo, hasa unapoongelea ccmagamba!
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hawezi kujiuzulu na nitasikitika akijiuzulu maana atakuwa anamsafishia njia yule Mwizi wa kimataifa kuwa Rais. Chiligati simkubali lakini kitendo chake cha kujitoa kwa hali na mali ili Lowassa asitimize malengo yake, niko upande wa Chiligati
   
 4. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Yeye unadai ametishia na wewe unaendelea kufikiri....................neither vitisho nor kufikiri are real
   
 5. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mmmmmmmmmmmmmmh---Chiliiiiiiigatiiiii.
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama anaweza kusimamia masuala anayoyaamini na afanye hivyo kwani atajijengea heshima. Wait a minute! mpaka hapo alivyokuwa anajibu hayo maswali ya Mwananchi amethibitisha kuwa Mdomo wake haupo pale matendo yake yalipo
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sasa anamtishia nani? Hivi huyu bwna ni muhimu sana kwenye chama kiasi kuwa ana uwezo wa kutishia?
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Majibu ya Chiligati kwenye red hakuna hata moja linaloonyesha kuwa ametishia kujiuzulu...Title ya thread yako haihusiani na ulichokisema.
   
Loading...