Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Baadhi ya kauli hizo ni ile aliyoitoa wakati wa hafla ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Kanisa Katoliki Changombe, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Sitta alisema ujasiri wake na maisha yake yanatokana na nguvu na ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Alisema nguvu hizo zimekuwa zikimwezesha kutekeleza wajibu wake kwa uhakika bila kuyumbishwa wala kuogopa kitu chochote.
Sitta ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akishambuliwa kwamba amewasaliti Watanzania kutokana na kuufunga mjadala wa kashfa ya Richmond, juzi akiwa mjini Songea, alikaririwa tena akisema alinusurika kuvuliwa uanachama CCM kutokana na ujasiri wake wa kusimamia ukweli.
Sitta alisema kauli kwamba alitaka kupokonywa kadi ya CCM kwenye vikao vya NEC mwaka jana na mwaka huu mjini Dodoma ni ya ukweli na kila mtu anajua. Huo ni ukweli wenyewe, tatizo liko wapi? Maana kila mtu anajua, mimi sioni kama kuna siri hapa, na hili nitaendelea kulisema hata kama wenzangu hawataki, alisema Sitta.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, aliiambia Tanzania Daima jana kuwa, CCM imeshangazwa na kauli za Sitta wakati anapaswa kujiandaa kwa usuluhishi, alisema kwa kawaida vikao vya NEC na CC ni vya siri na mjumbe yeyote hapaswi kutoa siri za vikao hivyo.
Ndugu yangu kweli nimemsikia, inasikitisha sana, lakini sina cha kusema na nakuomba uandike hivi kwamba Chiligati hana cha kusema kuhusu kauli za Sitta, alisema Chiligati.
Akizungumzia kauli za Sitta, Msekwa kama ilivyokuwa kwa Chiligati, alisema hawezi kusema chochote kwani kamati yao ni ya CCM na inafanya kazi za CCM na si za CHADEMA. Hii kamati ni ya CCM, si ya CHADEMA, ninyi watu wa CHADEMA mnaitakia nini? Hata kama Sitta anatoa kauli tata si kazi yetu, tuacheni jamani, mnaitakia nini CCM? alilalama Msekwa
Source: Tanzania Daima
My take
Kamati ya Mwinyi itaweza kweli kuleta suluhisho ndani ya CCM na Msekwa alijuaje mwandishi aliyekuwa anamhoji ni wa Chadema?