Twalb zubeir
Senior Member
- Feb 23, 2015
- 143
- 51
cc Chabruma, LizaboniAngekuwepo ndugu yako OKW BOBAN SUNZU angekusaidia. Ila inaonekana kala ban maana si kawaida yake
mda mwingine nakaa kimya natafakari,jinsi miaka mingine mi5 inavyopotea bila kuwa na rais.hili la CCM kumpa usukani abiria sio ishu sanaAngekuwepo ndugu yako OKW BOBAN SUNZU angekusaidia. Ila inaonekana kala ban maana si kawaida yake
Mbona Shein alikwisha kuvunja record yake, si alipata asilima 99.9Nakumbuka JK akimtambulisha Magufuli kwa wana CCM baada ya Magufuli kuteuliwa kugombea Uraisi kwa tiketi ta CCM alisema hivi:
" Hii ngoma ni ya mwali, na mwenye mwali ni mimi basi niachieni mimi" kilichofuata hapo ni Kampeni ya Kihistoria na ya kistaarabu iliyomuingiza Magufuli Ikulu bila hata kurusha bomu moja la machozi kwa Wapinzani.
Kwa heri baba JK, Hakuna tena mwanasiasa atakayekuja kupata kura asilimia 80 katika mazingira haya ya vyama vingi kama wewe Muheshimiwa.
Umelitendea taifa Makubwa, mabarabara, shule za kata, umeme wa REA, Taasisi ya moyo, Daraja la Kigamboni, Malagarasi, Dawa za ARV bure, Diplomasia ya hali ya juu, Jeshi bora lenye zana za Kisasa, Uhuru wa Habari na Demokrasia pana, Mishahara ya wafanyakazi iliyoboreshwa, Kada ya Wajasiriamali wadogowadogo, bodaboda, bajaji, mpesa, tigopesa, Umetujengea kituo cha michezo cha Kikwete Complex, Umeletea maji kutoka Ruvu chini hivi sasa shida ya maji DSM itakuwa ni historia, Mzee umetuwejea mradi wa Magari yaendayo Kasi DSM.
Asante sana baba JK, Tunakukumbuka na tutakukumbuka sana