Chiesa aondoka Liverpool

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
327
Reaction score
716
Mshambuliaji wa Liverpool, Federico Chiesa, mwenye umri wa miaka 26, huenda akaondoka klabuni hapo Januari iwapo atakosa muda wa kutosha wa kucheza baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha.

Winga wa zamani wa Manchester United, Jadon Sancho, yuko kwenye mazungumzo na angalau klabu mbili za Ligi Kuu ya England kuhusu uwezekano wa kujiunga nazo.

AC Milan inapanga kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Brazil, Endrick, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Real Madrid mwezi Januari.


Manchester United bado inamtaka kiungo wa Leicester City, Louis Page, mwenye umri wa miaka 18, baada ya kushindwa kumsajili siku ya mwisho ya dirisha la usajili.


Manchester City inaendelea kumfuatilia kiungo wa Atletico Madrid, Alex Baena, mwenye umri wa miaka 25, ingawa huenda klabu hiyo isifanye uhamisho wake Januari.

Liverpool na Manchester United zimewasiliana moja kwa moja na Wolves kuhusu uwezekano wa kumsajili winga mwenye umri wa miaka 18, Matheus Mane.

Brentford imeanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wake Mjerumani, Kevin Schade, mwenye umri wa miaka 24, katika jitihada za kuzuia Arsenal kumnasa.

Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 16, Isaac Konde.
 
We naye 🤣🤣🤣
Mimi shabiki wa Liverpool kinda kondakta umeniketea habari ya Chiesa kuondoka ninekushangaaa eti.

Kabla ya kupost habari ipitie kwanza sio una paste tu. Gossip na rumours
 
Yupo sana , sasa mbele ya Salah angepata nafasi ? Halafu huyu ni injury prone nakumbuka ligi ya Uingereza ina intensity ya hali ya juu kama goigoi utabaki kuwa Mchezaji wa wodini tu
Impact yake ni ndogo hata hivyo, akibaki au akiondoka hakutakuwa na hasara kwa upande wa Liverpool, sijaona impact yake kwa ukubwa sana pale Merseyside, hata kama Salah kaondoka, hawezi kuwa regular starter
 
Impact yake ni ndogo hata hivyo, akibaki au akiondoka hakutakuwa na hasara kwa upande wa Liverpool, sijaona impact yake kwa ukubwa sana pale Merseyside, hata kama Salah kaondoka, hawezi kuwa regular starter
Pengo la Salah lipo sana na halitozibika, tupo na dogo Rio na yule Munoz na tuna mpango wa kumsajili Olise wa Bayern. Chiesa nafasi yake ni ndogo hata kama kucheza namba 10 kuna Wirtz, Szoboszlai bado sana yule
 
Pengo la Salah lipo sana na halitozibika, tupo na dogo Rio na yule Munoz na tuna mpango wa kumsajili Olise wa Bayern. Chiesa nafasi yake ni ndogo hata kama kucheza namba 10 kuna Wirtz, Szoboszlai bado sana yule
Ndiyo nilikuwa nasemea kuhusu impact ya chiesa kwenye timu, kuhusu Salah hilo halina ubishi yeye ni miongoni mwa legends wa pale anfield na pengo lake kuzibika sio simple hivyo, ila tukimpata olise itakuwa njema sana maana ni feeder mzuri sana na uwezo wa ku hold mipira kwa muda mrefu, hii itasaidia sana kwenye mikimbio pamoja na kutengeneza nafasi, olise atatufaa sana na isak ataanza kuuwasha moto wake vzur kama hilo dili lita tiki
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…