MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,233
Shule ya wasichana pekee ya Chief Ihunyo inayochukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita turn iliyoko mkoani Mara wilaya ya Butiama eneo la Butuguri maalufu wa wenyeji wa wazanaki iliyojengwa na Mh Nimrod Mkono na kuikabidhi kwa serikali inaonekana ni tishio kwa matokeo mazuri kanda nzima ya Ziwa Victoria baada ya kuwa ya kwanza mkoani mara na pia ya kwanza kanda ya ziwa na ya 25 kitaifa...hii shule ni shule ya serikali lakini pamoja name kuwa na utitili wa shule binafsi kanda ya ziwa lakini imeonekana kuwa ni shule bora kuliko zote...hii shule ilijengwa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita tu kwa wasichana na ni bweni. Mkono alijenga shule mbili pamoja na ya Wavulana iitwayo Osward Mang'ombe science high school ambayo ni shule ya kidato cha tano na sita tuu. nayo ni shule ya bweni ambazo ziko majirani..lakini ya wasichana imekuwa tishio zaidi sijui ni kwa sababu ni shule ya Masomo ya art tuu au tofauti...lakini kama serikali imeboresha walimu wazuri katika shule hii basi serikali inabidi iiangalie shule hii nyingine ya wavulana ili kuiboreshea walimu bora wenye ujuzi zaidi wa masomo ya Sayansi..maana hii shule ya Osward Mang'ombe ina kila kitu cha kisasa.majengo ya kisasa, maabara ya kisasa lakini nadhani walimu wataalamu zaidi wanakosekana pale ili kuweza kutoa wanasayansi wazuri zaidi..maana rais Jakaya alienda kuzindua maabara ya kisasa pale ila kwann haifanyi vizuri?
Hongera Chief Ihunyo kwa kuonyesha mfano mzuri kwa shule za Serikali .
Hongera Chief Ihunyo kwa kuonyesha mfano mzuri kwa shule za Serikali .