Chid Benz: Mpaka sasa hivi Babu Tale ameshatumia zaidi ya milioni 40 kwa ajili yangu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
Moja kati ya watu anaowaheshimu rapa Chidi Benz, ni Babutale, kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa kwaajili yake.

xChidi.jpg.pagespeed.ic.D6IQ0ReUQb.jpg

“Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba Tale anaweza akawa ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo vimefanyika tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Tale anachokifanya anaonesha kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane kwenye suala la hela, nia yangu wewe uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’ Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini nachukulia kwamba yeye aone kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa miaka miwili but mimi sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza.

Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale kama familia yake.

“Kwasababu hata sasa hivi nakaa kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo hata ukija mkataba labda aniandikie miaka 20 kwamba haina maana.”

Tale alimsaidia rapper huyo kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka kuingia studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.
 
Anakaa na Tale, yaani yuko KWAO, ina maanisha Tale na mahela yote hayo bado yuko KWAO? (KWA WAZAZI). Ina maanisha vijana wwanaogopa kujitegemea au vipi?
 
Uongo mchana kwupe tale alipe 40m au 50m haha muuulizeni kayumba alifanywa nini na hawa waganga njaa
 
Bila shaka hizi ni zile pesa ambazo Babu Tale alizipata baada ya kuuza cd za mawaidha za yule ustadhi anayemdai milioni 200+. Ustadhi popote ulipo kaza buti pesa yako Babu Tale anayo.
 
Huyu bado arosto inamsumbua... Eti 60mil.. Chidy kwel kapoteza,juzkati kasema kua yeye ndo hip hop artist mwenye mafanikio kuliko wote... Mpuuuz sana hyu dogo
 
Moja kati ya watu anaowaheshimu rapa Chidi Benz, ni Babutale, kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa kwaajili yake.

xChidi.jpg.pagespeed.ic.D6IQ0ReUQb.jpg

“Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba Tale anaweza akawa ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo vimefanyika tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Tale anachokifanya anaonesha kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane kwenye suala la hela, nia yangu wewe uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’ Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini nachukulia kwamba yeye aone kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa miaka miwili but mimi sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza.

Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale kama familia yake.

“Kwasababu hata sasa hivi nakaa kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo hata ukija mkataba labda aniandikie miaka 20 kwamba haina maana.”

Tale alimsaidia rapper huyo kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka kuingia studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.

Naona Chid Benz bado hajapona vizuri kwani sijaona Rehab center ya kumgharimu hizo Pesa hadi sasa hasa ukizingatia pia na muda aliokaa na maisha ya huko. Angesema mpaka sasa Babu Tale katumia Shilingi Milioni 4 au hata 6 pengine kidogo ningemuamini. Na hili ndilo tatizo la Watanzania tunapenda mno " mashauzi " ya kipuuzi kabisa wakati uhalisia wake ni uwongo mtupu. Narudia tena kusema kwa aina hii ya uwongo naona Chid Benz bado hajapona vizuri tatizo lake la " kubwimbika ".
 
Jamani msisahau tabia ya wasanii Wa bongo kuongeza 0 kwenye vitu vyao milion 4 husema million 40. Msishangae sana ndiyo bongo yetu
 
Kama kweli katumia kiasi hicho ujue ni lazima utazilipa kwa namna yoyote ile iwe kufanywa punda au msukule
 
Back
Top Bottom