Chicken Wings zilizopakwa Mayai

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Mahitaji
Vipapatio vya kuku kilo 1
Yai 1, pasua na vuruga
Kikombe 1 cha unga wa ngano, kwa kuweka utando (layer) juu ya kuku
Kikombe 1 cha siagi (butter)
Mahitaji ya sauce

Vijiko 3 vikubwa vya soy sauce
Vijiko 3 vikubwa vya maji safi na salama
Kikombe 1 cha sukari
½ kikombe cha white vinegar
½ kijiko kidogo cha kitunguu saumu cha unga
Kijiko 1 kidogo cha chumvi

Maelekezo
Hizi chicken wings zinachovya kwenye mayai kisha kukaangwa kwa muda mfupi kwenye siagi. Baada ya kukaanga vinachovywa kwenye sauce na kisha kuokwa. Zikiiva utapata ladha tamu ya chicken wings laini na tamu.

Washa oven kwenye nyuzijoto 350 degrees F (175 degrees C), acha ipate moto.
Kata vipapatio vya kuku (chicken wings) katikati, chovya kwenye mayai na kisha chovya kwenye unga.

Hakikisha mayai na unga vimeenea vizuri.
Bandika chombo jikoni kwenye moto wa wastani, acha kipate moto kisha weka butter. Acha iyeyuke.

Weka vipapatio ya kuku na kanga hadi vibadilike rangi. Epua na weka kwenye waya wa kuokea.

Kwenye bakuli ya wastani, changanya soy sauce, maji, sukari, vinegar, kitunguu saumu, na chumvi. Koroga vizuri hadi mchanganyiko uwe sawia. Nyunyizia sauce juu ya vipapatio vya kuku.

Weka vipapatio kwenye oven, oka kwa muda wa dakika 30 to 45. Weka sauce juu ya vipapatio mara kwa mara. Vikiiva epua na weka pembeni.

Jirambe na ladha tamu ya japanese chicken wings.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom