Chezea mapenzi! Myahudi na mpalestina waoana

Chezea mapenzi! Myahudi na mpalestina waoana

Do santos

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
635
Reaction score
340
Mwanamke wa kipalestina (فلسطي&#1606😉 kutoka eneo Tulkarem kaskazini Mwa West Benk amefunga ndoa na Myahudi wa Israel ambaye amesilimu na kuwa muislamu .


Saedah Haroun, mwenye umri wa kati ya 30, anasema kwamba mume wake Dawood mwenye umri wa miaka ya 40, baada ya kusilimu alienda kujisajili mwenyewe kama muislamu katika mahakama ya Mamlaka ya Palestina .
Saedah aliongeza kwamba David alibadili jina lake na kuwa Dawood kama sehemu ya uongofu. Pia alibainisha kuwa kwa miaka mingi Dawood alikuwa na mahusiano mema na Waarabu na Waislamu katika Israeli,


Alisema kuwa katika miaka hii alikuwa amevutiwa zaidi na Uislamu, na hatimaye kukubalika kubadili dini kama sehemu ya ndoa yake.


Aliongeza kuwa wengi wa marafiki zake na familia walihudhuria harusi , na kusema kuwa ilikuwa ni " mbali na siri ," na kulikuwa na sherehe na furaha kama harusi
yoyote katika eneo lao.


Aidha, kumekuwa na wimbi la kusilimu kwa mayahudi wanawake na kuolewa na wanaume wa kipalestina. Mwezi septemba mwaka jana liliripotiwa tukio la kuvamiwa na kupigwa kijana na kiarabu na vijana watano wa kiyahudi karibu na maeneo ya Katamon huko Jerusalem, wakihisi kijana huyo ana mipango ya kumsilimisha na kumuoa.


Palestina ambao wanafata madhehebu ya Imam Hanafi, wanawake wa Kiislamu wanazuiwa kuolewa na watu wasio Waislamu .


Hata hivyo, Mtu anayesilimu huchukuliwa kama muislamu mwingine yoyote.
chanzo: www.ahbaabur.blogspot.com
 
Ni kweli mapenzi yana nguvu lakini linapokuja swala la kuabudu mtu anapaswa aamue yeye mwenyewe na kutoka moyoni anataka aabudu wapi anapooona ndipo kuna ukweli,lakini mtu anapoamua kuabudu sehemu fulani kwa ajili tu ya mapenzi sidhani hata kama atafauta misingi yote ya kuabudu sehemu hiyo kwa njia nzuri kama wanaoabudu kutoka moyoni.
 
Wayahudi wanatabia ya kusilim kwa minajili ya kuishi miongoni mwa Waislam ili wapate kuwapeleleza na kujua nyendo zao. Ndio maana wale walioua wanasayansi wa Iran kule Tehran hawajakamtwa hadi leo maana wauaji ambao ni Wayahudi anaishi miongoni mwa Wairan kama wananchi wa kawaida.

Kule Gaza Hamas wanaua watu wanaoshukuwa kuwa Wayahudi jiulize wanatoka wapi?

Hakuna shindi kwa uislam hapo hiyo ni mbinu ya muda mrefu ya Wayahudi
 
They know love We know love with attachments
^^
 
Back
Top Bottom